H-BABA YUPO TAYARI KUPAMBANISHWA
Mwimbaji H Baba ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa yeye ndiye mkali wa jukwaa aka mkali wa stage Afrika Mashariki na hakuna anaeweza kumfunika..
Akizungumza katika moja ya mahojiano yaliyofanywa kwenye kituo cha Times Fm, H. Baba alisema kuwa yuko tayari kupanda jukwaani kushindana na msanii yeyote ambaye anadhani ndiye mkali wa jukwaani na kwamba msanii huyo alipwe pesa yeye afanye bure kumthibishia.
“Hakuna kama H Baba kwenye stage na hakuna atakaenifikia mimi labda nife leo au kesho. Kama kuna msanii yeyote East Afrika anajua yeye ni mkali wa stage ajitokeze, mimi peke yangu na yeye peke yake. Mimi nitaperform bure yeye alipwe pesa.”
“Hata akama Tanzania kuna mtu anajijua yeye ni mkali wa stage peke yake asogee. Mimi nitaperforme peke yangu na kucheza na yeye vilevile.” H Baba ameiambia The Jump Off ya 100.5 Times Fm.
Ameongeza kuwa ameamua hivyo kwa sababu anaona kuna wasanii wanaopewa nafasi ya kuwa wakali wa jukwaa nay eye kuwekwa kando wakati hali halisi ni kwamba yeye ndiye mkali wao.