Inawezekana wewe ukawa ni miongoni mwa mashabiki wa nguli wa Hip hop rapper Scarface, na ulisikia taarifa ya kukamatwa kwake na polisi mara tu alipopokea Tuzo kutoka BET Hip Hop awards 2015.
Face alichukua tuzo ya I am Legend na alikamatwa mara tu aliporudi Backstage, taarifa ya awali ilidai Scarface alikamatwa kwa kosa la kushindwa kumuhudumia mtoto wake, pamoja na kuvunja agizo la polisi la kumtaka kutotoka ndani ya Jimbo la Texas.
Sasa rapper huyo kaamua kutoa maelezo yake, ambayo yameonyesha kukubaliana kuwa ni kweli alikamatwa na polisi mjini Atlanta, lakini kiasi kilichotajwa anadaiwa si sahihi.
Amekanusha kuwa hakukuwa na barua ya kumjulisha kuwa, hakutakiwa kuvuka ‘boda’ kwenda nje ya mji wa Texas na mara kadhaa amekuwa akienda Atlanta.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.