Google PlusRSS FeedEmail

DEF JAM IMETAJWA KAMA NDIYO LEBO YA HIP HOP ILIYOFANIKIWA ZAIDI DUNIANI

Wafanyakazi wa Def Jam inabidi wapige ‘Bata’ ndefu wiki hii, ni baada ya ‘lebo’ hiyo kongwe ya muziki kutajwa kama ndiyo lebo pekee ya Hip Hop yenye mafanikio muda wote.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtafiti Matt Daniels, ambae amepitia chati zote kubwa za muziki duniani, zimethibitisha kuwa Def Jam ndiyo imeingiza mikwaju mingi iliyokaa muda mrefu kwenye chati hizo.

Utafiti huo ulimrudisha mpaka mwaka 1989, na kulazimika kupitia lebo takribani 600 vigezo rasmi aliangalia lebo yenye Hits nyingi za Hip Hop, Usambazaji na mwelekeo.

Ifuatayo ni tano bora iliyopatikana, ikiongozwa na Def Jam.

1. Def Jam – 1925 cumulative weeks on the charts
2. Young Money – 1322
3. Roc-a-Fella – 1293
4. Jive – 1255
5. Bad Boy – 1060.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging