BARUA AILIYOANDIKA 2PAC $ 225,000
Mwaka 1995 wakati nguli wa Hip Hop duniani Marehemu Tupac Shakur, akiwa jela mjini New York aliandika barua kuwaasa vijana wenye asili ya kiafrika nchini Marekani.
Pac alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya Ubakaji, na barua hii aliiandika kwenda kwa Nina Bhadreshwar aliyekuwa muhariri mkuu kutoka Death Raw Uncut Magazine.
Shakur kupitia barua hiyo, alielezea jinsi ambavyo amechoshwa na maisha ya vurugu na utata, akifafanua kama kuna mwingine anaweza akaendeleza kwa kuwa yeye amechoshwa nayo.
Sasa barua hiyo inauzwa kwenye tovuti ya kumbukumbu, kwa kiasi cha dola za Kimarekani 225,000 ikiwa na kurasa tano zilizoandikwa kwa mkono wake mwenyewe.
Kikubwa katika barua hiyo alitaka kuwajulisha vijana levo ya maisha ya kutafuta aliyoyafikia, na kuwajulisha kuwa kuna levo zaidi ya hiyo.