Muigizaji nyota wa kundi la Emmerdale Charley,Webb juzi alionekana mwenye furaha baada ya kuhudhuria katika tunzo za Inside Soap zilizofanyika London DSTRKT,England.
Tunzo hizo ambazo hufanyika kila mwaka ziliwashirikisha wasanii mbalimbali wa filamu kutoka England ambapo nyota huyo alihudhuria na kuonyesha ujauzito wake kwa mashabiki
Nyota huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 27 alionekana kutokuwa na wasiwasi ingawa alionekana akiwa peke yake bila mpenzi wake..Katika tunzo hizo nyota huyo alifanikiwa kushinda tunzo ya msanii bora wa filamu wa mwaka ambapo pia aliwashukuru wadau mbalimbali waliomsaidia kupata mafanikio hayo katika tasnia hiyo..