Flora ndiye aliyefungua kesi hiyo baada ya kutokea mgogoro kwenye ndoa yao iliyosababishwa na kesi ya kudaiwa kubaka aliyoshtakiwa mumewe. Hata hivyo Emmanuel hivi karibuni alikuwa mtu huru baada ya kushinda.
Mwanasheria wa Flora, Edo November amedai kuwa wawili hao wamekubaliana kuifuta kesi hiyo kwaajili ya uhai wa familia yao yenye watoto wawili.
“Ninachoweza kusema ni kuwa yule ni mume wangu bado ninampenda,” “Tunamshukuru Mungu kwa hilo na kila mmoja amekuwa na amani ndani ya moyo wake,” aliongeza.
Mbasha alisema bado wana mpango wa kuikuza familia yao. Kuna tatizo moja lakini ili kufanikisha hili – Emmanuel Mbasha hayuko tayari kurudiana na mke wake!!