“Nimekuwa nikifanya utafiti wangu, [Tanzania] mna wasanii bora Afrika, sidanganyi kabisa,” alisema. “Nasubiri sana siku moja wote tuweze kukutana na kufanya wimbo mmoja mkubwa wa wasanii wa Afrika,” aliongeza.
Katika hatua nyingine Seyi alidai kuwa amemfollow Alikiba lakini yeye ameshindwa kumfollow na amemuomba afanye hivyo. Seyi Shay ni miongoni mwa wasanii waliosumbuliwa mwaka huu kutoa album na hivi karibuni ..Staa huyu amethibitisha kuwa Albamu yake inatoka November 2015.
Seyi Shay amesema album itaitwa “Seyi or Shay” na itatoka Ijumaa ya November 13, 2015. Kutakuwa na pati ya kusikiliza album na nyimbo zake kama ‘Irawo’, ‘Right Now’.