Google PlusRSS FeedEmail

KUTOJITAMBUA KUMETUA WASANII – BIGGIE

              

Msanii  wa filamu wa kiume Lumole Matovolwa ‘Biggie’ amefunguka kwa kusema kuwa sababu kuu ya soko la filamu kudorora ni kutokana na wasanii wengi kutokujitambua, ikiwa ni pamoja na kutokuwa makini katika utengenezaji wa kazi za sinema nchini.

“Kushuka kwa soko la tasnia ya filamu limetokana na sisi wasanii wenyewe kwa kumtegemea mfanyabiashara achukue kazi zetu na atutangaze, pili kukosekana kwa sera ya filamu iliyokaliwa na wenye nchi, tunakuwa maskini kila kukicha,” Biggie.

Aidha Biggie amesema kwa hivi sasa mtayarishaji wa filamu akitengeneza leo hata akimaliza uhariri akipeleka sokoni kazi hiyo hawezi kulipwa kwa wakati kwani malipo utolewa kwa nadra sana, biggie anasisitiza Serikali kuleta sera ya filamu hiyo ndio mkumbozi wa shida za wasanii.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging