Star wa Hip Hop Bongo Izzo Business, ametoa mtazamo wake na sifa za Rais atakayekwenda kumchagua Octoba 25 mwaka huu.
Akizungumza kupitia kipindi cha The Jump Off Izzo amesema Rais ajaye anatakiwa awe muelewa wa kuangalia nyanja za ujambazi zilizoongezeka, jinsi atakavyofufua viwanda vilivyo kufa.
“Mimi napenda kwanza nimtambue kama baba, maana sisi ndio tunakuwa kama watoto kwake, aweze kutuongoza wanae kuyafikia maendeleo zaidi, atatue tatizo la Ajira, Aongeze kasi ya kiuchumi na kuangalia sekta ya viwanda.
“Unajua sasa hivi ukiangalia ujambazi umeongezeka kwa sababu vijana hawana ajira, kwa hiyo awe tu baba mwenye uelewa wa mambo mengi” Alisema Izzo.
Katika ‘line’ nyingine, mkali huyo kutoka Mbeya alifafanua kwanini hashiriki katika kampeni kwenye uchaguzi wa mwaka huu, amedai anaogopa kuwagawa mashabiki wake katika makundi.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.