Mwimbaji wa kike Bongo Flever Khadija Said amesema hana mpango wa kwenda nje ya nchi kutengeneza video za nyimbo zake kama wanavyofanya baadhi wa wasanii hapa nchini Tanzania \
Alisema haoni sababu yoyote na ya msingi kwa maana hata hapa kuna watengenezaji wa video bora kama hizo za huko nje
Msanii huyo ambaye ametamba vilivyo na wimbo wake'' Maumivu'' alisema kuwa ni vyema wasanii wakathamini kazi zinazoandaliwa nchini badala ya kifikiria tu kwamba hazina ubora