Muigizaji Nick Cannon amesema kwa sasa ana furaha baada ya kumpata mpenzi mpya anayejulikana kama Samatha Johnson
Cannon alisema hayo wakati akizungumza na gazeti moja nchini marekani..alisikika akisema ''nina furaha sana ,nina amani ya moyo sasa mara baada ya kuachana na mke wake Mariah Carey.
Alisema furaha hiyo imerejea baada ya kuanza uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo huyo hivi karibuni
''ukweli sasa kichwa changu kimetulia ,nilikuwa kwenye kipindi kigumu baada ya kuachana na mama watoto wangu''alisema
Cannon alisema Samatha ni mrembo ambaye ana mvuto kama alivyokuwa kwa Mariah na sasa ana maisha yenye furaha.