Baada ya wiki kadhaa za furaha ya nyota wa muziki nchini Marekani,Tyga kumnunulia mpenzi wake Kylie Jenner,Gari aina ya Marcedes G Wagon alipofanya katika sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake,hali imebeadilika na kuwa ya huzuni
Uhusiano wa wawili hao unaonekana kuingiwa na mdudu mbaya baada ya kutokea malumbano kati yao ambapo kwa mujibu wa mtandao wa Hollywood Life,chanzo ni kwamba Tyga alimtukana mpenzi wake huyo kwa kumfananishana Drake.
Mtandao huo umeeleza kwamba Kylie alimhoji Tyga kwamba hataki kusikia mashabiki wakiimba baadhi ya nyimbo zake anapokuwa baa kama anavyoimbiwa Drake.,ndipo sintofahamu ikaanzia hapo ,Tyga akaona amefedheheshwa