Habida ambaye alijitosa katika fani ya muziki baada ya kuachia ‘Sunshine’ na kisha kufuatisha na kolabo nyingine ‘Reason’ aliyomshirikisha Cannibal ziliochangia pakubwa kumweka katika ramani, amekuwa kimya kwa muda sasa katika tasnia.
Hata hivyo hii imetokana na sababu kwamba amekuwa Marekani kwa muda wa wiki mbili sasa, tangu alipoachia kazi yake mpya ‘Keep On Walking’.
Habida yupo Marekani kwa ajili ya ziara za kisanii na ni kwenye mojawepo ya pitapita zake katika jiji la Atlanta kwenye shughuli zake hizo hivi majuzi ndipo alihusika kwenye ajali mbaya ambayo ilisababisha gari lake kuharibika vibaya sana hasa kwenye boneti.
Lakini kikubwa zaidi ni kwamba Habida alinusurika ajali akitoka akiwa mzima mzima ila pengine tu hofu ndiyo itakayokuwa ikimsumbua.
Taarifa hizi Habida alizithibitisha mwenyewe baada ya kuposti picha la gari lake hilo lililobondeka bondeka na kisha kuandika chini yake, “Mwanzo wa ziara yangu Atalanta umeanza kwa mkosi. Ila ninashukuru nimebarikiwa, nilinusurika ajali na nipo mzima wa afya kabisa”