Kweli kama wasanii wakongwe kuwepo katika game ndio wanaua soko la filamu, toka nakua nimekuwa nikisikia wasanii kama Angelina Jolie ana filamu bado zinauza, kwangu wagombea wa Urais wana deni la kulipa,”anasema Monalisa.
Monalisa anaenda mbele zaidi kwa kusema kuwa serikali imeshindwa kusimamia soko la filamu kwa kuachia filamu kutoka nje zisizo na stempu kuuzwa hovyo bila kulipa kodi na kubanwa kazi za ndani, lakini hivi sasa wasanii ndio wanatumika katika kusaka ushindi bila msaada kwao.