Mkali wa muziki wa Bongo Flava Seif ‘Matonya’ shaaban, ameuelezea wimbo wake wa ‘kitambo’ Vailety kuwa ndio wimbo uliompatia pesa nyingi kwa haraka.
Akizungumza jana kupitia kipindi cha ‘The Jump off’ cha Times FM, Matonya anasema wiki kadhaa tu baada ya kuiachia ngoma hiyo, alikutana na ‘mpunga’ mkubwa kwenye akaunti yake Benki.
“Vailety aisee was crazy song kiukweli, ulikuwa wimbo mkubwa sana, nilipokea simu nyingi kutoka Marekani na kwenginepo, yani ulipagawisha watu kiukweli.
Sasa sikuwahi kushika hela nyingi yani, pesa zangu nyingi zinaingia benki tu, sasa ile siku natazama akaunti naona kama milioni 150 hivi afu kwa haraka tu yani” alisema Matonya.
Katika ‘line’ nyingine, Tonya Time alikiri kuwa ‘mkwaju’ huo ulimpatia maadui wengi sana.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.