Mshindi wa Tunzo za Grammy Rapper Kanye West na Rapper Jay-Z wanatarajiwa kutoa alabamu ya pamoja ambayo itakuwa na ngoma tano za ukweli na tayari wameshaweka bayana jina albamu hiyo wameibatiza jina Watch the Throne.
Kanye West aliongeza kwa kusema wazo la albamu hiyo ya pamoja ni la wote wawili ambapo swala hilo lilikuja siku moja walipokuwa wamekaa wakijadiliana kuhusu muziki wao kwa ujumla ndio chanzo cha chimbuko la albamu hiyo Watch the Throne,
Sisi wote ni wakali na hakika kila mtu anajua kote ulimwengini na sasa ni wakati wa kuwaunganisha mashabiki wa Big Boss wangu Jay Z na mashabiki wangu,kupitia albamu hii ambayo itakuwa na nyimbo tano kali...
Tumeanza kuandika mashairi ya nyimbo zote tano leo August 27 na tumeanza kuandika wimbo utakaokuwa wa pili katika albamu yetu..na wimbo huo tumeupa jina Happy Good Friday