Baada ya kimya cha muda mrefu na kukumbwa na maralia kali,hatimaye Chery Cole ,juzi alionekana akiingia studio mjini Los Angeles,Marekani,
Chery aliyekuwa mke wa mchezaji wa Chelsea Ashley Cole,alikumwa na ugonjwa wa maralia alipokuwa mapumzikoni hapa Tanzania..
Hata baada ya kurudi nchini Uingereza kimwana huyo ambaye ni mwanamuziki kutoka katika kundi la Girls Aloud alizirai ghafla akiwa kwenye shughuli za ujaji katika mchezo w x Factor
Juzi alionekana akiwa mwenye bashasha ,chery alionekana akiwa anateremka kwenye gari na kwenda moja kwa moja studio kwa ajili ya kufanya kazi yake ya muziki,
Imeelezwa kuwa kimwana huyo anataka kurecord nyimbo zake mpya ambazo alitaka kuziachia kabla ya kuugua malaria kwa takribani wiki nne zilizopita,
Awali kabla ya kwenda Los Angeles,Chery mwenye umri wa miaka 27 alimwambia jaji mwenzake Simon Cowell kwamba anakwenda mapumzikoni nchini Tanzania...
Lakini imeripotiwa kwamba Chery tayari amesharecord kibao kipya ambacho anatarajia kukitambulisha kwenye onyesho la pili la X-factor
Video ya kibao hicho inatarajiwa kurekodiwa wiki ijayo ambapo mwanamuziki huyo,ameshafanya majaribio kwa muda wa saa nne...