Google PlusRSS FeedEmail

SNOOP ATAKA WATOTO WAKE NA DAVID BECKHAM KUIMBA PAMOJA

Mwanamuziki mkongwa wa hip hop snoop dog,amesema yuko katika mipango ya kumtengeneza kimuziki mtoto wa kwanza wa mcheza soka David Beckham,


Watoto hao wa kiume wa mwanasoka huyo Brooklyn mwenye umri wa miaka 11.atakuwa ni mmoja kati ya watoto watakunda kundi vijana wadogo ambalo litamshirikisha mtoto wa Snoop Dogg,Corde mwenye umri wa miaka 16..na Cordell 12 na watoto wengine wa Beckham ni Romeo na Cruz.


Imeelezwa watoto wa mwanasoka huyo hawajakuwa na mwamko wa fani yoyote tangu walipozaliwa na kama wangejaliwa vipaji ambavyo wanavyo wazazi wao wangeku tishio kwa sasa.


Corde na Cordell wanataka kuingia katika fani ya muziki na kama wataunganika na watoto wa Beckham watapata mafanikio makubwa sana..


Snoop ameshaongea na wanamuziki kama Bow Wow na Soulja Boy na kuwataka kuwafundisha watoto hao namna ya kuimba na mambo mengine ya muziki,na wamekubaliana na ombi hilo  na wamekubali kufanya nyimbo za pamoja na watoto hao...


Snoop Alikaririwa akisema angependa sana kundi hilo liwe na nyimbo zenye mahadhi kama nyimbo zinazoimbwa na  mwanamuziki mdogo kutoka Canada Justin Bieber..

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging