Google PlusRSS FeedEmail

FILAMU INAYOELEZEA MAISHA YA MVUMBUZI WA MTANDAO WA FACEBOOK NA CHANGAMOTO ZINAZOMKABILI KUTOKA KWA WADAU WA MTANDAO HUO

Hii ni sinema inaonyesha maisha ya muazilishi na mvumbuzi wa mtandao wa kijamii unaotumiwa na watu wengi duniani ujulikanao kama FACEBOOK.

Kijana aliyekuwa anasoma katika chuo kikuu cha Harvard mnamo mwaka 2003 kijana anajulikana kama  Mark Zuckerberg ni mtalamu wa program za kompyuta alikuwa amekaa chumbani kwake na kompyuta yake na akijaribu kuja na wazo litakalo ubadilisha ulimwingu katika njia ya kuwasiliana.

Ambacho alikianzisha chumbani kwake kikaja kuwa mtandao wa kijamii wa dunia nzima. Ndani ya miaka sita tu na ukiwa na marafiki au watumiaji zaidi ya milioni 500 kijana huyu amekuwa bilionea mdogo katika historia ya binaadam , lakini katika ngazi hiyo ya ujasiriamali mafanikio yanampelekea katika migongano binafsi na ya kisheria, Je atapambana nayo vipi?

Usikose sinema hii ambayo inatoa changamoto nzuri kwa vijana. Itakuchua mda wa masaa mawili tu kuona kijana huyu alifikiria nini mpaka kuamua kuvumbua FACEBOOK ambayo mpaka mabosi ofisini wanaipiga marufuku wafanyakazi waachane na mtandao huo bila mafanikio,watu wameanzisha mauhusiano mpaka ndoa na wengine uhusiano ama ndoa zinakufa kutokana na mtandao huu..tafuta nakala yako...

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging