Google PlusRSS FeedEmail

CELINE DION ATARAJIA MAPACHA WA KIUME



Mwanamama na pia ni Mwanamuziki kutoka nchini Canada Celine Dion yuko karibu na madaktari wake kwa sasa kwa maana mda wowote anaatarajia kujifungua watoto mapacha,tena wa kiume, The Associated Press limeripoti

Akiwa na umri wa miaka  42 sasa yuko katika hospitali moja inayojulikana kwa jina  St. Mary’s Medical Center ambayo iko huko West Palm Beach, Florida nchini Marekani,aliongeza kwa kusema kuwa karibu na madaktari kwa mama mjamzito ni vyema kwa kila mama mjamzito anapokaribia kujifungua ni vizuri kuwa karibu na vituo vya afya ili mama aweze kujufungua salama..na huu utakuwa uzao wa 2 kwa mwanamama huyo kwa maana tayari ana mtoto mmoja na mumewe Rene Angelil na mtoto wao Rene Charles ana umri wa miaka 9 sasa..


Mnamo mwezi  August 2009, mwanamama Celine Dion alitangaza hadharani kuwa yeye ni mjamzito wa mtoto wake wa pili ila mimba yae ilipofikia umri wa miezi sita kwa bahati mbaya mimba hiyo ilitoka na ndio maana kwa sasa ameamua kuwa karibu na madktari ili kuepusha balaa kama lililomtokea mwaka jana

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging