Google PlusRSS FeedEmail

HATIMAE RAPPER T.I ATUPWA LUPANGO KWA MARA NYINGINE

T.I. atatumikia miezi kumi na moja gerezeni, hukumu hiyo ilitolewa siku ya ijumaa pamoja na mwanamuziki huyo kuwa katika kipindi cha maangalizi.

T.I amehukumiwa kifungo hicho ikiwa ni baada ya kukutwa na hatia ya kumiliki madawa ya kulevya huko katika jiji la Los Angeles mwezi uliopita akiwa na mkewe Temika. Ikumbukwe wakati anakutwa na skendo hiyo ilikuwa ni miezi michache tu ametoka jela kutokana na kosa la kumiliki silaha isiyokuwa na kibali.

Siku 2 kabla ya hukumu hiyo T.I alikuwa amesaidia polisi katika kumshawishi mtu aliekuwa anataka kujiua kwa kujirusha toka gorofa ya 22 asifanye hivyo, ingawaje kitendo hicho watu walikichukulia kama jamaa anajitengenezea mazingira ya kuonekana ni kijana mzuri mbele ya macho ya jaji

Ukisoma file la rapper huyu utagundua kuwa amekuwa na tabia ya kukamatwa na madawa ya kulevya toka miaka ya 1998.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging