Mwanadada Mwasiti Almasi ndio anakuwa news ndani ya ukurasa huu wikiendi hii,ambapo anasema yupo katika dakika za majeruhi kudondosha albamu yake mpya na ya pili mara tu baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Akichonga na vuvuzela letu, Mwasiti alisema albam hiyo itakuwa na jumla ya pini 8 ukiwemo ule unaendelea kutamba hivi sasa kwenye vituo vya redio cha 'Si Kisa Pombe' alioimba kwa kushirikiana na rapa Quick Racka.
"Kwa sasa najiandaa kufyatua albamu yangu mpya ya pili ambayo itakuwa na nyimbo nane na nimerekodi kwenye studio tatu za Ngoma Records, Fishcrab ya Lamar na Sound Crafters ya Enrico," alisema Mwasiti.
Mwasiti alisema pamoja na maandalizi ya kuiachia albamu hiyo kuendelea vyema, hadi sasa bado hajaamua aiite kwa jina gani, kwa maelezo kwamba anaendelea kutafuta jina litakalovutia sokoni.
Mwasiti toka kundi la THT, alianza kutamba mara baada ya kuachia wimbo uliotamba wa 'Haooo' kabla ya kufyatua vibao vingine kama 'Niambie,' 'Huruma', 'Nalivua Pendo'. Albamu yake ya kwanza aliita 'Niambie'.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








