Wasanii maarufu kutoka Marekani TPain, Elephant, Gyptian na Mims wanatarajiwa kupamba katika tamasha kubwa la Str8 Muziki linalotarajia kufanyika Novemba 27 katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.
Meneja wa chapa ya SM wa kampuni ya Sigara Tanzania Tanzania (TCC) Isamba Kasaka alisema kuwa mbali na wakali hao pia kutakuwa na wasanii wengine wa Afrika Mashariki.
Kasaka alisema kabla ya tamasha hilo kutatanguliwa na mengine mawili ambako moja litafanyika Novemba 13 katika eneo la Magadu Morogoro na la pili litafanyika Novemba 20 katika ukumbi wa Royal Village mjini Dodoma.
Aidha Ksaka alisema wasanii wengine watakaopamba katika matamasha hayo yenye lengo la kuwakutanisha pamoja wanajamii ambao ni pamoja na Michael Ross (Uganda), Fid Q, Mwana FA, Joh Makini, Chegge na Sam wa Ukweli.
Mwaka jana tamasha hilo lilimleta msanii kutoka Nigeria D Banj pia liliwahi kuwaleta wakali kama Eve, Fat Joe, Maya, Shaggy, WayneWonder, Malaika na Sean Paul.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








