Google PlusRSS FeedEmail

JD AWANIA TUNZO ZA PEARL OF AFRICA MUSIC AWARDS

Mwanamuziki bora wa kike kwa mwaka wa 2009/10 kwa mujibu wa tunzo za muziki za Tanzania, Kili Awards,hapa namzungumzia....Judith Wambura Mbibo Habash, amerudi kitaani kusaka mashabiki wake kwa hali na mali, katika kuhakikisha kwamba anaongeza tunzo nyingine ya muziki kwa mwaka huu, safari hii akiisaka nafasi hiyo kutoka nchini Uganda.

Jide ambaye ni mwanamuziki pekee wa kike nchini anayeonesha kufanikiwa waziwazi kutokana na kazi zake anazozifanya, ametajwa kuwania nafasi ya mwanamuuziki bora wa kike kutoka Afrika Mashariki kupitia tunzo za kila mwaka zinazofanyika nchini Uganda, ambazo zimebatizwa jina la pearl of Africa Music Awards.

Kutokana na tabia ya mashabiki wengi wa kitanzania kumpenda mtu akiwa jukwaani tu na kusahau kila kitu baada ya kuondoka pale, Jide ameamua kutumia blog na kila anapokuwa kwenye maonesho, akimaliza kutumbuiza wimbo mmoja, huhamasisha mashabiki, wamsaidie kurudisha tuzo nyumbani ambayo italeta heshima kwa Taifa pia.

Katika debe lake hilo mwanadada amewasisitiza watanzania kuchukua simu zao na kuandika ujumbe wa maneno unaosema 36, na kisha wautume kwenda namba + 256 752 600 100 

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging