Google PlusRSS FeedEmail

UZURI NA UREMBO SI TIKETI YA KUOLEWA

Kim Kardashian mwanamama ambaye kila kukicha anazidi kujipatia umaharufu mkubwa sana katika ulimwengu wa burudani 
Mwanadada huyu si mwimbaji wala mcheza filamu. Akiwa na umri wa miaka 30 sasa na mafanikio makubwa katika ulimwengu wa kibiashara kuanzia maswala ya urembo, matangazo ya kwenye tv na majarida mbalimbali pamoja na utengenezaji wa vipindi vya televesheni  (Reality tv shows), lakini yeye mwenyewe anadiriki kusema kuwa hajui nini kime msibu mpaka sasa hana mafanikio katika maswala ya kimapenzi.

“Nilidhani ningekuwa nimeshaolewa na sasa nina familia yangu lakini sikama nilivyodhani kumbe mambo hayako huvyo. Kwa mimi mafanikio ni kupata mume anaekujali kwa kilakitu na kuwa na familia bora na hicho ndio nitakacho endelea kukitafuta kila siku” aliliambia jarida la PEOPLE. Wakati akiyasema hayo ndugu zake ambao ni Kourtney 31 pamoja na Khole 26 wameshaolewa na Kourtney ana mototo mmoja na ukilinganisha kiurembo na mvuto Kim bado anawazidi wenzie..

Mwandada huyu amekuwa na balaa ya kutokaa na wapenzi kwa mda mrefu ambapo maisha yake ya nyuma kabla ya kufikisha umri wa miaka 30 yeye anasema alikuwa anatumia nguvu nyingi sana katika mahusiano na kuhakikisha penzi linakuwepo.
Akiongeza adai imekuwa kama miujiza ukizingatia mimi ndio nilikuwa mda mwingi nipo katika mapenzi zaidi ya wezangu na sasa kibao kimegeuka mda huu mimi ndio niko bila mtu, naona kuna kitu kimekosekana katika maisha yangu najaribu kujituliza ilinipate ambae atanifaa maishani mwangu..

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging