Google PlusRSS FeedEmail

ANTI VIRUS VOL 2 HIYOOO NI KWA AJILI YA MAFISADI NA WAZEMBE KATIKA NYADHIFA MBALI MBALI ZA SELIKALI

Baada ya kukamilisha kazi waliyoahidi ya kumkampenia hadi kufanikisha msanii mwenzao Joseph Mbilinyi ‘Mr II au Sugu’, kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, wasanii wa kundi la Wagosi wa Kaya, wamebainisha kuwa sasa wanakuja na ‘Anti Virus Vol 2’.
Fred Maliki ‘Mkoloni’ mmoja wa wasanii wa kundi hilo, anachana live bila chenga kuwa, kundi hilo limeamua kuendeleza harakati zao, hivyo hawatachoka kupiga kelele kulalamikia ufisadi au kupinga huduma mbovu, hadi wahusika watakapojirekebisha.

Alisema, ni kutokana na uamuzi huo, ndio maana wameamua kutoa sehemu ya pili ya wimbo wao huo, lengo likiwa kuwakosoa viongozi na watendaji wasiotimiza wajibu na dhamana walizopewa.

“ baada ya kufanikiwa kukamilisha kampeni zetu kwa ndugu yetu Sugu, sasa tunarejea katika kampeni zetu dhidi ya mafisadi, hatutachoka , tumeachia albamu mpya ya Anti Virus Vol 2,” alisema Mkoloni.

Alisema, wamepania kuisambaza kila pembe ya nchi, ili kila Mtanzania popote alipo aweze kuipata kazi hiyo ambayo imebeba ujumbe mzito.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging