Baada ya kufanya vizuri akiwa na kundi sasa anakuja mwenyewe na tayari ameshaachia singo inayokwenda kwa jina la Oooh akiwa ameshirikisha msanii kutoka nje aitwae Jade
G Nako ambaye anasema singo hiyo ni uatambulisho wa albamu yake ya kwanza itakayokuwa na nyimbo nane tu lakini kali.
"Nakuja na albamu yangu itakayokuwa na nyimbo nane, tano nimekwisha zitengeneza na nyingine tatu ziko jikoni zinapikwa, zikiwa tayari naingiza albamu sokoni"alisema.
Hata hivyo amesema maandalizi ya albamu yake hayajaathiri yale ya kundi ambayo nayo yanaendelea hivi sasa.
"Nipo kazini kotekote, nikiwa na kundi nakamua mpaka mwisho na nikiwa solo mwendo ni huohuo, mashabiki wangu na kundi wanalijua hilo," alisema Nako.
Nako alisema kama ikitokea leo mtu akamuuliza anunue albamu ipi pale ya kwake na ya kundi zikiingia mtaani alisema, " Ukimpenda G Nako, utawapenda Nako2Nako Soldiers, so hapo itabidi tu ununue albamu zote ili ufaidi" alisema Nako.
Nako ambaye Ooh ameifanya chini ya B Hits akiwa na Pancho Latino lakini sasa anamalizia mzigo chini ya Sababisha Records
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








