Ahmed Ally 'Madee' amewataka wadau wa muziki kumuunga mkono bwana mdogo aliyekuja kwa kasi kwenye miondoko ya hiphop,nchini Dogo Janja. Madee amemuelezea Dogo Janja kama msanii wa kweli na makini kutokana na kazi yake kuifanya kutoka moyoni tofauti na wasanii wengine
Wanaochipukia(Underground). "Wanaojua muziki wanaweza kumkubali kwa kazi zake na hata katika uimbaji wake kutokana na kuwa tofauti na wasanii wanaoibukia" alisema Madee.
Mpaka sasa Dogo Janja amesharekodi track mbili ambayo ni 'Anajua' na 'Mtoto wa Uswazi" ambazo kwa kiasi kikubwa zimekubalika.
Hata hivyo Madee alisema dogo Janja kwa sasa atakuwa akifanya zake kazi kwa awamu kutokana na majukumu yake ya shule.
Alisema Dogo tumempeleka shule kutokana na umri wake ili aweze kujiendeleza zaidi pamoja na kujipanga katika suala la elimu kwani leo yupo Tip Top kesho anaweza kuwepo sehemu nyingine kimaisha.