Google PlusRSS FeedEmail

CHELEA MAN ALONGA KUHUSU MUZIKI WAKE

                Chelea_man_face
Mwanamuziki aliyejizolea umaarufu mkubwa kipindi kile cha mvumo wa muziki wa kizazi kipya cha Mb Dogo, Chelea Man anatarajiwa kuibuka tena upya kwenye Industry ya muziki wa Bongo Fleva baada ya kutojitambua kwa muda mrefu jambo lililompelekea kuwa na wakati mgumu na kuisusa gemu kwa muda.
Mwanamuziki huyo anasema kwamba alikuwa akiimba lakini hakujua thamani yake, kwani watu walimtumia sana kwa manufaa yao, huku yeye akiambulia kiduchuu jambo ambalo alipokuja kuligundua roho ilimuuuma sana na kujikuta akikimbilia migodini hukooo, kwaajili ya kutafuta maisha mengine.
Anasemaaliamua kwenda kwenye kuweka kambi yake hiyo huko migodo ya Barick huko pande za Kahama akiwa na shughuli za kutafuta dhahabu.
Hata hivyo amesema baada ya kutoka hapo, alikwenda Uganda kidogo, na rafiki yake ambapo alijipatia mafunzo ya muziki na ndipo alipojitambua vizuri na kuturudi tena jijini Dar es salaam kwaajili ya kurudisha heshima yake kwenye muziki.

KWA HISANI YA MUDDY BONGO 5

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging