
Katika taarifa yake aliyoitoa katika vyombo vya habari wiki hii,Oge amesema madai hayo siya kweli na yamelenga kuchafua jina lake.
Oge amesema amechoka kupokea simu ma meseji nyingi kutoka kwa ndugu,jamaa na rafiki zake wakimuuliza iwapo taarifa hizo zilizotolewa na vyombo vya habari ni za kweli.
"Mimi na mume wangu wiki chache zilizopita tulisherehekea siku ya kuzaliwa ya motto wetu wa mwisho,hivyo sielewi kwa nini watu wanaeneza tuhuma ambazo hazipo,’’alisema.
’Najisikia vibaya ninaposoma hizi na inaonekana kama yupo Oge Okeye Mwingine .Mimi nipo salama hakuna chochote kilichotokea baina yangu namume wangu,’’aliongeza.
Oge alisema ndoa yake haijawahi kukumbwa na matatizo yoyote na kusisitiza kuwa ,mumewe na wifi zake wanafurahia maisha yao na kumwonyesha upendo mkubwa.
Amewataka waandishi wa habari na wanaoeneza uvumi huo kwenda kutafuta kazi zingine za kufanya ili wawe bize kwa sababu yeye na mumewe hawana muda wakupoteza kusoma taarifa zao.
Oge amesema anatarajia kuigiza filamu mpya hivi nkaribuni ,ambayo picha zake ztapigwa nchini Canada.Pia alisema aqmepata nafasi ya kucheza filamu na waigizaji kadhaa nyota kutoka Hollywood.







