
BAADHI ya waongozaji wa filamu wa Ghana awmemtaka mcheza sinema wa kinigeria,Tonto dikeh amwombe radhi Van Vicker ,vinginevyo asahau kucheza filamu za nchi hiyo.
Van vicker ni mmoja wa watu wanaoheshimika katika tasnia ya filamu nchini humo Hivyo hawako tayari kuona akidhalilishwa kwa namna yoyote ile.
Uamuzi huo wa waongoza filamu umekuja baada ya kuwepo na taarifakuwa, Tonto na van Vicker,ambao wana uhusiano wa kimapenzi,walipigana wakiwa
Kwenye eneo la kutengeneza filamu. "HIvi unaweza kumdhalilisha RMD kama vile,’’ alihoji mmoja wa ongoza Filamu hao,ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Wameonywa kuwa watamfungia mwongoza filamu yeyote, ambaye
Atamshilikisha Tonto katika filamu yake. Pia wamesema wamesema wataandika barua malalamiko kwa chama cha waigizaji Filamu wa Nigeria.
Hadi sasa, Tonto hajasema lolote kuhusu onyo hilo na iwapo atakuwa tayari Kumwomba radhi Van Vicker.
Mzozo kati ya Van Vicker ulianza wakati wa mazoezi ya upigaji wa picha za Filamu yao mpya,ambapo kila mmoja alikuwa akifanya mazoezi kivyake. Baada ya mwongozaji wa filamu hiyo kugundua kasoro hiyo,aliamua kuwafuata Kwa lengo la kuweka mambo sawa,lakini Tonto alionekana kupandwa na hasira na
Kuanza kusema hovyo. Hali ilikuwa mbaya baada ya Tonton kuwasha sigara na kumpulizia moshiVan VIcker ,ambaye kwa sauti ya upole, alimwomnba aache kufanya hivyo ama aende kuvutia nje.Toto aliichukulia kauli hiyo ya Van Vicker kama kumtusi na kuanza kumtusi ya nguoni.







