
Mwanamuziki Ryan Adams 36 alipotangaza kuachana na muziki wa bendi na kuamua kufanya muziki wa kujitegemea.
Mkali huyo wa miondoko ya Rock & Roll kwa sasa yuko katika wakati mgumu kimuziki kutokana na kusumbuliwa na maumivu makali ya sikio,ambayo yamemsababishia kutosikia
"Umefika wakati sasa wa kupumzika maana ugonjwa huu unanisumbua sana na kwa muda sasa"
Ryan Adams ambaye alikuwa katika bendi ya Whiskytown alijiengua katika bendi hiyo mnamo mwaka 1999 na kuamua kufanya kazi zake binafsi.
Mwaka mmoja baadae alifanikiwa kutoa albamu iliyojulikana kama Heartbreaker Albamu hiyo iliweza kufanya vyema na alifanikiwa kutoa albamu nyingine akishirikiana na bendi ya The Cardinals,Na kwa sasa ameipua albamu nyingine ambayo inafanya idadi ya vigongo 13 ambavyo ametunga yeye mwenyewe







