
Mtengenezaji wa filamu ya Madness of King George amepanga bajeti kubwa kwa ajili ya kutengeneza filamu mpya ambayo itakuwa ikizungumzia maisha ya aliyekuwa mke wa Princess Charles ,Princess Diana..Stephen Evans Producer ambaye alipata mafanikio makubwa kupitia filamu ambazo amezifanya hapo awali kama Madness of King George ambayo aliifanya mwaka 1994 nyingine ambayo ilimpatia umaharufu na fedha nyingi ni filamu Twelfth Night na The Wings of the dove..Yuko katika maandalizi ya kutengeneza filamu hiyo tangu mwaka 1997
Kiasi cha paun million 31.2 kinatarajiwa kutumika kwa pesa ya kwetu ni sawa na shillingi Billion 63
Filamu hiyo itaonyesha jinsi Princess Diana alivyoomba talaka yake mwaka 1996, maisha yake mara baada ya ndoa yake







