Kufuatia kuwa kimya kwa miaka kadhaa,mwanadada Jojo yuko katika harakati za mwisho kumalizia albamu yake mpya ambayo ameipatia jina la Jumping Trains,muimbaji huyo amesema anatarajia kuachia albamu yake hiyo mapema mwakani 2012..
Mara baada ya kuachia single ya kwanza rasmi,ambayo aliipa jina la Disaster kwa ajili ya albamu hiyo ,Jojo amesema anatarajia wimbo wake mwingine uitwao "Elsewhere ambao anatarajia utafanya vyema katika Albamu yake hiyo mpya..Jojo katika albamu yake iliyopita alitamba na vibao vyake kamatoo little too late na vingine vingi..








