Wakati wimbo wake “Sauti ya Jogoo” ukiendelea kujaribu kuamsha Watanzania, bila shaka watu wengi wanataka kufahamu kitu gani hasa kilimsukuma Nikki Mbishi kuandika wimbo kama ule mashairi mazito yaliyowasilishwa kwa utulivu na mpangilio wa hali ya juu.
Nikki alisema haya: “Nilikuwa nawaza kuongelea uhalisia wa tasnia ya siasa Tanzania inavyojenga matabaka baina ya watu wa ‘chini’ na wa ‘juu’. Na pia nilitaka kuwakumbusha watu majukumu yao kama jogoo awaamshavyo waliolala alfajiri inapojiri.