Msimu wa wasanii Tanzania Kuvuna Walichokipanda kati ya mwaka 2011 maana Tunzo pekee Nchini Zijulikanazo kama Basata Kilimanjaro Music Awards zimewadia na tayari mchakato huo umezinduliwa rasmi ..Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa, wanamuziki waliofanya vizuri mwaka jana kwa ajili ya kupewa tuzo mwaka huu, watachambuliwa kwenye Academy ya siku mbili kama ambavyo hufanyika kila mwaka.Taarifa kwa vyombo vya habari, iliyosomwa na meneja wa kampuni wadhamini wa Kili Music Awards, George Kavishe imeeleza kwamba kwenye academy ndipo wanamuziki watapagwa kwenye vipengele (categories) tofautitofauti.Kavishe alisema, academy itafanyika kati ya Januari 26 na 27 ambapo wadau kati ya 50 na 100, watakutana na kuchanganua wanamuziki wa aina zote, waliofanya vizuri mwaka jana na kuwekwa kwenye vipengele vyao kabla ya kuruhusu Watanzania wapige kura kuwapata wale watakaotunukiwa tuzo hizo.Alisema, kura za Watanzania zitabeba uzito wa asilimia 70 na majaji 15 watakaa kama jopo na kusimamia watu watakaoshinda ili wawe ni wale kweli wanaostahili.Alifafanua kwamba uzito wa kura za majaji 15, ni asilimia 30....
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.