Kenya au Bongo, Nchi gani ipo vizuri kwenye burudani ya muziki? Jibu la swali hilo litapatikana Februari 5, 2012, wakati masupastaa wawili, David Mathange ‘Nameless’ kutoka Kenya, atakapopambana jukwaani na Mfalme wa Temeke, Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature
Mpambano huo wa aina yake, utachukua nafasi kwenye ukumbi mkubwa wa kisasa, Dar Live, uliopo Mbagala Zakhem, Dar es Salaam.Mbali na shoo hiyo ya mpambano wa mastaa hao wakubwa Afrika Mashariki na Kati, kutakuwa na burudani tofauti kusindikiza mpambano huo.Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Kundi la Taarab la Mashauzi Classic na burudani nyingine nyingi zitasindikiza mpambano huo “Itakuwa shoo ya aina yake, Nameless atataka kuthibitisha kuwa yeye ni mwanamuziki wa kimataifa, wakati Nature na kundi lake zima la TMK Wanaume Halisi, wataonesha kuwa wao ndiyo wakali wa kazi. Mbali na hilo, watoto wataburudika kwa michezo yao kama kawaida ya Dar Live,” alisema Mratibu









