Mtayarishaji wa muziki
wa kizazi kipya,P-Funk – aka majani amesema kwa sasa yuko katika mipango
ya kufanya kazi na wasaniiwa kimataifa akizungumza jana na pro-24,amesema
kwanza atafanya kazi na wasanii wan ne kutoka marekani.wimbo wa kwanza
natarajia kufanya na J-cole anayetumia lebo ya Jay Z Ila nitakuwa nikifyatua kazi za wasanii wa kimataifa kila
mwezi.Aidha amesema kwa hapa nchini msanii chid benz ameshakamiliasha albamu
yake na wako katika hatua za mwisho kuingiza albamu hiyo sokoni..
Kuhusu taarifa za kuanzisha kampuni ya kurekodi video
amesema yeye hataki kujihusisha na video bali ataendelea na kuandaa kazi za
audio peke yake..aliongeza kwa kusema “huwezi ukawa mchezaji wa michezo miwili
tofauti na ukawezakufanya vyema ni sawasawa na wahenga kusema mshika mawili
moja humponyoka”..








