Google PlusRSS FeedEmail

PROFFESOR JAY AAMUA KUISHI NA MAMA YAKE MZAZI

Mwanamuziki Profesa Jay amhamishia mama yake mjengoni kwake Baada ya kuhamia kwenye mjengo wake wa kifahari uliopo Mbezi Mwisho, Dar es Salaam, staa wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, amemhamishia mama yake Kabla ya Jaya hajachukua uamuzi huo, mama yake alikuwa anaishi kwa tabu kutokana na nyumba yake kuathiriwa na mabomu, Gongo la Mboto, Dar es Salaam, mwaka jana.
Jay alisema, alisubiri kuona serikali ikichukua hatua ya kutengeneza nyumba za waathirika lakini baada ya kuona hali ni kimya, aliamua kumnusuru mama yake.
“Niliona mama anahitaji kuondolewa kule haraka. Uvumilivu wangu kwa serikali ulikuwa siyo kitu kabisa,
“Kwa sasa mama kurudi Gongo la Mboto labda mpaka serikali ikishamtengenezea nyumba yake na kwa hali halisi ilivyo, hilo halionekani kama linaweza kufanywa leo wala kesho,” alisema Jay.

KWA HISANI YA DEIWAKA

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging