Mkongwe wa Hip Hop, anayepewa heshima ya kuwa muasisi wa Bongo Fleva, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ atawaongoza wanaharakati kibao katika shoo babkubwa itakayofanyika kwenye Klabu ya New Maisha, Januari 29, mwaka huu.Mratibu wa shoo hiyo, Fred Mariki ‘Mkoloni’ amesema kuwa katika shoo hiyo, itakuwa muafaka kusikiliza mawe yaliyomo kwenye mixtape za Anti Virus volume I na II...Alisema, shoo hiyo ni mwanzo tu, kwani nyingine nyingi zitafuata kwa sababu wamepewa shavu la miezi sita kwenye klabu hiyo.Aliongeza kwamba kwa kuanzia, Januari 29, watafanya shoo baadhi ya Vinega wakiongozwa na Sugu, kisha mwezi ujao, watapiga kazi wengine.Aliendelea kusema kuwa Januari 29, mbali na Sugu, wengine watakaoshika mic ni Mapacha, Anselm Ngaiza ‘Soggy Dog’, Suma G, Daniel Kamili ‘Dani Msimamo’, Happy Thadei ‘Sister P’, DJ Snox wa Mabaga Fresh na Mkoloni mwenyewe.Alisema kuwa ndani ya Club Maisha, itakuwa muafaka kumwaga mistari ya Anti Virus mwanzo mwisho na Vinega wote wamejipanga kwa ajili ya kazi hiyo...
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








