Google PlusRSS FeedEmail

ALBAMU MPYA YA BARNABA ITAKUWA NA NGOMA KUMI NA ITATOKA JUNE MWAKA 2012

Mwanamuziki Barnaba amesema albam yake mpya itakayokuwa na jumla ya nyimbo 10, ambayo inatarajia kukamilika mwezi wa sita mwaka huu.''Unajua katika ndoto zangu za kimuziki nimekuwa na ndoto siku nyingi ya kurekodi na mastaa wa ukweli Duniani, na Fally ni mwanzo tu kwani wapo wengine ambao tayari nimeshawasiliana.,ambao wanatokea nchi za Magharibi ambao tayari wasanii wawili wakali wa R&B wamekwisha nithibitishia kunipa 'shavu' katika miongoni mwa nyimbo zangu kadhaa ambazo nyingine zitakuwa ni katika albam yangu ijayo baada ya hii.Hata Fally pia alikuwa akitamani kurekodi na mimi tangu nilipo mpagawisha katika moja ya shoo yake alipokuja nchini na kuipenda sauti yangu, kwa hiyo naye pia ni nafasi yake ya pekee aliyokuwa akiitamani ambayo amefanikiwa'' alisema.Barnaba alisema kuwa mbali na wimbo huo lakini pia anatarajia kurekodi video ya wimbo huo, awapo nchini humo iwapo atafanikiwa kumaliza ndani ya muda uliopangwa na mwandaaji wake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging