Google PlusRSS FeedEmail
Showing posts with label NEW. Show all posts
Showing posts with label NEW. Show all posts
Hali ya Miley Cyrus imeendea kuimarika siku kadhaa baada ya kulazwa hospitali na tayari ameanza kupanda jukwaani kupiga kazi, lakini mwimbaji huyo amelitosa jukwaa la shindano la kuimba la The Voice.

Kwa mujibu wa RadarOnline, chanzo kimesema kuwa mwimbaji huyo ameamua kuitosa dili ya kuimba kwenye fainali za shindano hilo kwa kuwa hampendi Christina Aguilera ambaye ni kocha wa shindano hilo.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa ingawa Christina Aguilera hayupo kwa muda kwenye shindano hilo bado Miley Cyrus hataki kusapoti kitu ambacho kinauhusiano nae hivyo hawezi kufanya show kwenye jukwaa hilo.

“Hata kama Christina hayupo kwenye show hiyo kwa muda, The Voice bado ni show yake na Miley hataki kunyoosha kidole chake kumsaidia mwanamke huyo.” Kimenukuliwa chanzo hicho.

Imelezwa kuwa mwezi uliopita ma-boss wa The Voice walimpa dili Miley Cyrus lakini aliwapa jibu la moja kwa moja kuwa hataweza kufanya show hiyo.

RadarOnline imeeleza kuwa chanzo cha hasira za Miley Cyrus kwa Christina Aguilera ni tweet yake aliyoiandika kuhusu show ya Miley Cyrus ya mwezi February ambayo alifanya akiwa amevaa kivazi cha aina yake kinachovaliwa na cowbos ‘Chaps’ .

Tweet ya Christina Aguilera ilimsifia Miley huku ikimng’ata kiana kuwa yeye (Christina) ndiye alikuwa wa kwanza kufanya show na kivazi hicho. Kitu ambacho kilimuudhi Miley Cyrus.

“Cheers from one dirrty girl to the next @MileyCyrus...wear em' loud & proud, girl-yes! (sic).” Ilisomeka tweet ya Christina.

MILEY CYRUS ALITOSA SHINDANO LA THE VOICE

Hali ya Miley Cyrus imeendea kuimarika siku kadhaa baada ya kulazwa hospitali na tayari ameanza kupanda jukwaani kupiga kazi, lakini mwimb... [Read More]

Msanii wa vichekesho 'The comed' Masanja Mkandamizaji pamoja na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Shilole wameula kwa kupata dili la maana ulaya

MASANJA NA SHILOLE WAULA ULAYA

Msanii wa vichekesho 'The comed' Masanja Mkandamizaji pamoja na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Shilole wameula kwa kupata... [Read More]







Msanii wa filam nchini Juma Kilowoko 'Sajuki' amefariki Dunia jana katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa ajili ya Matibabu , msanii huyo ambaye aliugua kwa kipindi kirefu alianza matibabu nchini na baadaye kupelekwa India.

Mei 13 mwaka jana Sajuki alienda nchini India kutibiwa baada ya kupatwa na maradhi ya tumbo na uvimbe katika ini na alianza matibabu katika Hospitali ya TMJ, Msasani, Dar es Salaam nakufanyiwa uchunguzi ambapo Hospitali hiyo ilithibitisha kwamba ili kufanikisha matibabu yake lazima apelekwe India lakini alishindwa kuifanikisha tiba hiyo kutokana na kushindwa gharama za matibabu kuwa kubwa.

Msanii huyo aliweza kupata fedha za matibabu kwa kuchangia na wadau pamoja na wasanii wa filamu nchini na kuweza kufanikisha safari yake ya kwenda nchini Indi kwa ajili ya matibabu

Sajuki aliweza kufika nchini India kwa ajili ya matibabu na baada ya muda aliweza kurejea nchini huku afya yake ikiendelea kuimarika siku hadi siku

Katika hali isiyo ya kawaida na ambayo haikutarajiwa siku za hivi karibuni msanii huyo alianguka jukwaani mjini Arusha wakati akijaribu kuwasalimia mashabiki, Sajuki alidondoka mjini Arusha alipokuwa anafanya tamasha kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa kumchangia pamoja na kutafuta fedha nyingine ili aweze kurejea India kwa ajili ya matibabu yake mwezi uliopita.

Sajuki alirudishwa jijini Dar es Salaam na kufikishwa katika hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam ambapo ripoti ya madaktari iliyothibitishwa na viongozi wa TAFF ilionesha kuwa msanii huyo amepata tatizo la kufeli kwa figo yake.

Kutokana na hali ya msanii huyo kuzidi kuwa mbaya ndugu pamoja na viongozi wa TAFF waliamua kumuhamishia msanii huyo katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya uangalizi zaidi huku mipango ya kutafuta fedha za kumpeleka tena nchini India zikiwa zinaendelea.

Rais wa Shirikisho wa Filamu Tanzania Simon Mwakifamba (TAFF) alithibitisha kuwa safari ya maandalizi ya msanii huyo kwenda India ilikuwa imekamilika baada ya Serikali kukubali kugharamia gharama zote za kumsafirisha

Alisema mpango wa kumsafirisha huyo kwa ajili ya matibabu ulikuwa umeshakamilika kilichokuwa kikisubiliwa ni msanii huyo kupata nafuu na awe na uwezo wa kupumua bila ya kutumia mashine

Alisema kuwa asingeweza kusafirishwa na mipira ya kupumua na hiyo ndio ilikuwa ni sababu ya wao kusubili mpaka atakapopata nafuu

"Pamoja na jitihada zote tulizozifanya kuhakikisha tunaokoa maisha ya msanii mwenzetu zimeshindikana kwani mungu alimpenda zaidi na asubuhi ya leo  Sajuki ameiaga Dunia,"alimaliza kwa kusema Mwakifamba huku akionekana  ni mwenye huzuni kubwa.

Msiba huo umepokelewa kwa hali ya majonzi na masikitiko makubwa kwa baadhi ya wasanii wa filamu nchini, viongozi wa siasa pamoja na wadau mbalimbali , ambapo wamesema ni pigo kubwa kwenye tasnia hiyo


Naibu waziri wa wizara ya Mawasiliano January Makamba ni mmoja wa wanasiasa walijitokeza kwenye kufanya mchakato wa kumchangia Sajuki ili aweze kuikamilisha safari yake ya kwenda India kwa ajili ya matibabu.

" Kwa mara ya kwanza mimi niliingia studio kufanya nyimbo ya kuhamasisha na aliweza kupata matibabu na kuweza kupata nafuu, nilikaa naye na nikamsikiliza alikuwa anandoto nyingi za kupeleka sanaa katika ngazi ya kimataifa " alisema Makamba

Makamba alisema kuwa wakati Sajuki alipokuwa kwenye hali mbaya alijitahidi kwa kila hali kwa kuhakikisha kuwa anaweza kupona na kurudi tena katika hali yake ya kawaida lakini imeshindikana kwani Mwenyezi Mungu ameamua kumchukua.

Alisema kuwa mbali na juhudi za watu wengine walishuhudia juhudi zake  mwenyewe binafsi kwa kuiangaikia afya yake ingawa kila jambo mungu ndio anayepanga.


Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe "Hali ya Afya ya Sajuki ndiyo ilinisukuma sana kuanza kusaidia wasanii nchini kupata kipato stahili cha kazi zao." aliongezea kuwa  "Kifo chake kimeniondolea Mtu niliyemtazama kama kishawishi Cha Mimi kupigania haki za Watanzania walio kwenye (entertainment industry),"alisema Kabwe.

Mbali na hayo katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Ghonohe Materego alisema kifo cha msanii huyo ni pigo kubwa kwenye tasnia ya filamu kwa kumpoteza msanii mahiri wa filamu

Alisema kuwa anatoa pole kwa familia ya Sajuki pamoja na wanafilamu kiujumla kwa kipindi kigumu walichonacho hivyo wanatakiwa wawe na moyo wa kushukuru kwa kila jambo.

Alitoa wito kwa wasanii wote ili kuwaenzi wapendwa wao ni lazima wayaenzi na kuyaendeleza mambo yote mazuri yaliyoachwa, kwa kufanya hivyo watakuwa wamewaenzi kwa vitendo.

Wakati huo huo msanii wa filamu Steven Nyerere alisema taarifa ya kifo cha msanii Sajuki amezipokea kwa mshtuko mkubwa kwani wamefunga mwaka kwa majonzi ya kuondokewa na wapendwa na kufungua tena mwaka kwa hali hiyo hiyo ya majonzi.

Alisema kuwa kila jambo linapangwa na mungu kwani sajuki aliumwa kwa muda mrefu na kauli yake ya mwisho ndio ambayo inamuumiza tangu alipopokea  taarifa za msiba wake.

"Steve  ndugu yangu nateseka sana bora nikapumzike", hii  ndio ilikuwa kauli yake ya mwisho kwangu inaniuma sana kwani tulijitahidi kupigania uhai wake ila mungu ndio kampenda zaidi" alisema Steve Nyerere

Steve aliongezea kuwa kwa hali hiyo yeye inamtisha sana kwani hajui itakuaje siku zijazo kutokana na mapigo yanayowakumba wanafamilia ya tasnia ya filamu mfululizo.


Naye msanii wa filamu Ray alitoa majonzi yake kwa kusema kuwa walijitahidi kuupigania uhai wake hata kwa kuwa naye bega kwa bega kwenye matamasha yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili ya kuchangia fedha za matibabu

Ray alisema kutokana na mapigo hayo wanayoyapata katika tasnia hiyo mungu anawakumbusha kwa njia hiyo wasanii kumrudia mungu, wamche mungu na kujiweka tayari muda wowote kwa jambo lolote lile.

Aliongezea kuwa wasanii wanatakiwa kumcha mungu na wasiwe watu wa starehe na kufanya hanasa, hivyo wanatakiwa kujua wanajukumu kubwa la kumcha mungu kila siku.

Naye Msanii wa Ushairi Tanzania Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba alisema kila mtu mwenye nyongo lazima atapokea taarifa hiyo kwa majonzi makubwa.

Alisema kuwa watanzania walionyesha juhudi kubwa ya kutaka kuokoa na kuupigania uhai wa Sajuki ila ndio imeshindikana hivyo ni pigo kubwa kwa wasanii na kwa watanzania kwa ujumla.

Mrisho aliongezea kuwa kuna kila sababu ya kutafakari matendo yao kwani kifo kinatumika kutukumbusha wajibu wetu na kuyaacha ya duni kwa kumrudia mungu

Marehemu  Sajuki alizaliwa mwaka 1986 mkoani Songea na ni mtoto wa nne katika familia yao na ana elimu ya kidato cha nne ambayo aliimaliza mwaka 2003 na alifika jijini Dar es Salaam mwaka 2005 na kuanza shughuli zake za kisanii ambazo aliendelea nazo mpaka mauti yanamfika.

Msanii huyo anatarajiwa kuzikwa kesho kutwa saa tano katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina!.


SAJUKI KUZIKWA IJUMAA, MAKABURI YA KISUTU

Msanii wa filam nchini Juma Kilowoko 'Sajuki' amefariki Dunia jana katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa... [Read More]



PRODUCER wa muziki wa kizazi kipya Charles Francis C9 ambaye pia ndiye aliyemuibua marehemu Shalo Milionea anatamani kufanya kazi na Lady Jay Dee kwa sababu ya uwezo aliyonao msanii huyo

Alisema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa anaelezea mikakati yake ya mwaka ujao jinsi ya kuboresha na kuendelea kuwa mbunifu katika kazi zake

Alisema kutokana na kipaji na uwezo aliyo nao msanii Jay dee anatamani siku moja afanye naye kazi na anaamini itakuwa ni kazi nzuri ambayo watanzania wataipokea na itafanya vizuri katika soko la muziki ndani na nje ya tanzania

Alisema kuwa si kila msanii mwenye jina au ambaye teyari ameshapata mafanikio anatamani kufanya naye kazi bali ni msanii pekee mwenye uwezo na nidhamu katika kazi ndiye anayempa kipaumbele kwanza

"Natamani sana kufanya kazi na Jay Dee kwa sababu ya kipaji chake ni kikubwa mbali na kipaji chake pia anaheshima katika kazi kitu ambacho kinanifanya niweze na nitamani kufanya naye kazi siku moja " alisema C9

Aliongezea kuwa wasanii ili wafike hatua ya maendeleo hususani wa muziki wanatakiwa wawe na heshima ya muda na kazi kwani kwa kutofanya hivyo wtakuwa wanajirudisha nyuma kimaendeleo wenyewe

Pamoja na hayo alielezea kuwa yupo mbioni kuendeleza mipango yao ya kazi ambayo walikuwa nayo kabla marehemu Shalo Milionea kufariki ikiwemo ya kusaka watu wenye uwezo wa kuimba stairy ailiyokuwa anafanya marehemu






C9 ATAMANI KUFANYA KAZI NA LADY JAY DEE

PRODUCER wa muziki wa kizazi kipya Charles Francis C9 ambaye pia ndiye aliyemuibua marehemu Shalo Milionea anatamani kufanya kazi na Lad... [Read More]

MUONEKANO MPYA WA BARNABA KATIKA VIDEO YAKE MPYA

Huyu ndiyo Barnaba mpya akiwa na muonekano wa tofauti katika video yake ya wimbo wa 'Sorry', mtindo wa nywele na aina ya mav... [Read More]




Mahakama ya rufaa leo inatarajia kuanza kusikiliza pingamizi za kuchunguza umri wa msanii maarufu wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’

Maombi hayo yatasikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Jaji Benard Luanda, Jaji January Msoffe na Jaji Katherine Oriyo

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo anadaiwa kumuua msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu Sinza Vatican Dar es Salaam

Umri wa msanii huyo umezua utata baada ya mawakili wanaomtetea kudai kuwa ana miaka 17 na si 18 kama hati ya mshtaka inavyoonyesha , na kuomba kesi yake isikilizwe katika Mahakama ya Watoto

Mahakama Kuu ilikubali kuchunguza umri wa mshitakiwa huyo lakini siku iliyotajwa kuanza kufanyiwa uchunguzi wa umri halali wa mshatakiwa huyo upande wa mashtaka uliitrifu mahakama hiyo kuwa umewasilisha Mahakama ya Rufaa maombi ya marejeo ya uamuzi huo

Jaji Fauz Twaib ndiye aliyotoa uamuzi wa kukubali kuchunguza umri huo lakini kutokana na upande wa mashtaka kuwasilisha maombi yao mahakama ya rufaa aliahirisha kuendelea na uchunguzi wa umri wa msanii huyo hadi Mahakama ya Rufaa itakapotoa uamuzi wake

PINGAMIZI ZA LULU KUSIKILIZWA LEO

Mahakama ya rufaa leo inatarajia kuanza kusikiliza pingamizi za kuchunguza umri wa msanii maarufu wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’... [Read More]





Wasanii washauriwa kujiheshimu na kuwa na heshima juu ya kazi zao za sanaa ya muziki ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea

Skendo za kila siku kwenye baadhi ya vyombo vya habari haziwezi kumjenga msanii katika soko la muziki la kimataifa bali inachangia kumboboma na kuvunja heshima yake kwa wadau na mashabiki wake wa muziki

Wasanii wanatakiwa kuwa na uongozi utakao waongoza na kuwapa mafunzo nini maana ya sanaa ili waweze kuheshimu kazi zao

Kauli hiyo ilitolewa na msanii anayetikisa katika anga za muziki wa kizazi kipya nchini Barnabas Elias ‘Barnaba’alipokuwa akieleza kuhusu uzinduzi wa staili yake mpya ya uimbaji inayoambatana na muonekano wa mavazi pamoja na aina ya nywele

Alisema kuwa mashabiki wake watarajie kumuona Barnaba wa tofauti kuanzia mavazi mpaka uimbaji hii yote katika kuboresha kazi ili zionekane zina ubora

Aliongezea kuwa kwa kuwa anaheshimu kazi zake pamoja na kuwajali mashabiki wake hufikiria vitu vyenye ubora zaidi katika kazi zake

WASANII WASHAURIWA KUJIHESHIMU

Wasanii washauriwa kujiheshimu na kuwa na heshima juu ya kazi zao za sanaa ya muziki ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea Sk... [Read More]

Wachezaji filamu maarufu Brad Pitty 48 na mchumba wake ambaye pia ni mcheza filamu wa Marekani Angelina Jolie 37 maarufu kama ‘Brangelina’ wameweka oda ya pete za dola mbili zenye thamani ya euro 500,000,kila moja kutoka kwa sonara maarufu Chanzo cha habri kilisema wako bize kutengeneza pete hizo za dhahabu na Almas zitakazofanana kwa wanandoa hawo watarajiwa,chanzo hicho kilibainisha kwamba Brad Pitt wiki iliyopita alimnunulia Angelina Jolie saa yenye thamani ya Euro 250,000 ambayo ni moja ya saa ya gharama duniani kama zawadi ya mpenzi wake kabla ya harusi yao ambayo itafungwa hivi karibuni ,wachumba hao wanawatoto sita kwa kipindi cha mahusiano yao kati ya watoto hao watatu ni wa kwao na wengine wamewaasili

BRAD PITT NA ANGELINA JOLIE KUCHONGA PETE EURO MIL 1

Wachezaji filamu maarufu Brad Pitty 48 na mchumba wake ambaye pia ni mcheza filamu wa Marekani Angelina Jolie 37 maarufu kama ‘Brangelina... [Read More]

NI zaidi ya miaka mitatu sasa tangu Chris Brown amtende kitu mbaya girlfriend wake wa wakati huo, Rihanna mwaka 2009 na bado nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ameshindwa kumfuta kwenye maisha yake Brown. Tayari ameshirikiana naye katika nyimbo mbili mpya mwanzoni mwa mwaka huu, ambayo inawaweka mashabiki kwenye mazingira mgumu.Hivyo kwa nini Rihanna anashindwa kumkunjia ndita moja kwa moja bwana wake huyo wa zamani. Katika toleo la Mei, mwaka huu la jairda la Elle, mwimbaji huyo wa wimbo mkali unaotetemesha, We Found Love amefunguka kiasi cha kutosha kwa nini amerudisha mawasiliano na bwana wake wa kale, pamoja na yote aliyomfanyia. "Naheshimu wanayosema watu wengine. Kikubwa ni kwamba kila mtu anafikiria kivyake," Rihanna amesema. "Ni vigumu sana kwangu kukubali, lakini napokea. Watu wanaishia kupoteza muda wao bure kwenye mablog au popote, wanahangaika, na yote sawa tu. Siwachukii kwa hilo,” alisema. Lakini Rihanna anabakia na msimamo wake juu ya kutomtupa Brown katika maisha yake — na hana mpango wa kuomba msamaha kwa hilo. "Kwa sababu kesho nitaendelea kuwa yule yule,"alisem. "Bado nitaendelea kufanya ninachokitaka." Ni kwamba mwimbaji huyo amekubali kwamba amejifunza mengi sana katika kipindi kigumu — na sasa yuko jasiri kwa ajili ya hilo. "Imenipa mtutu," alisema. "Nilikuwa kama, poa, k**a. wanafahamu zaidi kuhusu mimi zaidi ya ninavyotaka wajue. Inakera lakini hiyo ilitokana na uwazi wangu. Huo ulikuwa uhuru wangu, wakati wa kutoa hilo. Nilitaka watu wajue mimi ni nani. Vyovyote walivyolichukulia, vizuri au vibaya, nilitaka wajue ukweli." Na wakati akiendelea kubaki kuwa mtu maarufu katika macho ya watu, Rihanna anajihisi huru kuliko alivyokuwa daima kabla.

RIHANNA AJITETEA KUFANYA KAZI NA BROWN.

NI zaidi ya miaka mitatu sasa tangu Chris Brown amtende kitu mbaya girlfriend wake wa wakati huo, Rihanna mwaka 2009 na bado nyota huyo m... [Read More]

Kwa wakazi wa Mkoani Iringa Lile Bonge la Party ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu  kubwa hatimaye siku masaa sasa yametimia.Party hilo ambalo linajulikana kama Jeans Party litafanyika na ndani ya Club V.I.P Iringa mjini..kwa kiingilio cha sh 5000/=Tu.Burudani itaanza saa tatu kamili za usiku na show itasimamiwa vyema na mavijanaa wa Pro-24 Djs....USIKOSE UHONDO HUU,PIGILIA JEANS UJE NA MWENZIO TUJIMWAE PAMOJA.....MPAKA KUKUCHE..

JEANS PARTY NDANI YA CLUB V.I.P IRINGA LEO JUMAMOSI

Kwa wakazi wa Mkoani Iringa Lile Bonge la Party ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu  kubwa hatimaye siku masaa sasa yametimia.Party hil... [Read More]

Mwanamuziki Barnaba amesema albam yake mpya itakayokuwa na jumla ya nyimbo 10, ambayo inatarajia kukamilika mwezi wa sita mwaka huu.''Unajua katika ndoto zangu za kimuziki nimekuwa na ndoto siku nyingi ya kurekodi na mastaa wa ukweli Duniani, na Fally ni mwanzo tu kwani wapo wengine ambao tayari nimeshawasiliana.,ambao wanatokea nchi za Magharibi ambao tayari wasanii wawili wakali wa R&B wamekwisha nithibitishia kunipa 'shavu' katika miongoni mwa nyimbo zangu kadhaa ambazo nyingine zitakuwa ni katika albam yangu ijayo baada ya hii.Hata Fally pia alikuwa akitamani kurekodi na mimi tangu nilipo mpagawisha katika moja ya shoo yake alipokuja nchini na kuipenda sauti yangu, kwa hiyo naye pia ni nafasi yake ya pekee aliyokuwa akiitamani ambayo amefanikiwa'' alisema.Barnaba alisema kuwa mbali na wimbo huo lakini pia anatarajia kurekodi video ya wimbo huo, awapo nchini humo iwapo atafanikiwa kumaliza ndani ya muda uliopangwa na mwandaaji wake.

ALBAMU MPYA YA BARNABA ITAKUWA NA NGOMA KUMI NA ITATOKA JUNE MWAKA 2012

Mwanamuziki Barnaba amesema albam yake mpya itakayokuwa na jumla ya nyimbo 10, ambayo inatarajia kukamilika mwezi wa sita mwaka huu.... [Read More]

Mwanamuziki wa Muziki wa Pop George Michael afya yake  sasa imeanza kuimarika ,kwa mujibu wa mtandao wa Tmz kupitia mahojiano na Mmoja wa Madaktari wake…Mwanamuziki huyo alilazwa Vienna ,tangu Novembee mwaka jana akisumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na alikaa kwa muda wa mwezi mmoja hospitali bila kurusiwa kutoka..Lakini aliporudi Jijini London hali yake ilizidi kuwa mbaya na kulazwa tena.Lakini kwa sasa afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku..

GEORGE MICHAEL AANZA KUPATA NAFUU

Mwanamuziki wa Muziki wa Pop George Michael afya yake  sasa imeanza kuimarika ,kwa mujibu wa mtandao wa Tmz kupitia mahojiano na Mmoja wa... [Read More]

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Khamis Mwijuma Mwana Fa,amewataka wasanii wenzake ambao wamepata mafanikio katika sanaa hiyo,wabadilike na kutunga tungo za maana ili mda wote wawe kileleni..Mwana Fa alisema hayo wakatia akiongea na Pro-24 Mwishoni mwa wiki wakati akiwa katika mapumziko yake ya mwisho wa wiki..Aliongeza kwa kusema sasa kunawasanii wapya wengi na wanaimba huku wakiwa wamebana pua na wengine wanaimba huku wakitumia style ya vichekesho zaidi na kila siku zinavyozidi kwenda wanazidi kujizolea mashabiki….

FA.ATOA USHAURI KWA WASANII WENZAKE

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Khamis Mwijuma Mwana Fa,amewataka wasanii wenzake ambao wamepata mafanikio katika sanaa hiyo,wabadi... [Read More]

Mwanamuziki Lady Jaydee ameondolewa kwenye orodha ya wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza katika tamasha la sauti za Busara litafanyika kuanzia Februari 8 hadi Februari 12 mwaka huu huko Unguja Zanzibar taharifa hii imetolewa na mratibu wa tamasha hilo bwana Yussuf Mahmoud,amesema Jaydee alikuwa atumbuize katika tamasha hilo baada ya kuthibitishwa katika orodha ya awali..Yussuf Mahmoud amesema wamepokea taharifa kutoka kwa mume wa mwanamuziki huyo ambaye pia ndio meneja wake Bwana Gardner Habash kuwa Jaydee hataweza kutumbuiza kutokana na ushauri wa Dactari wake kuwa amemtaka apate mapumziko katiaka kipindi kisichopungua miezi mitatu.Mpaka sasa Haijaelezwa mwanamama huyo anaugua ugonjwa gani..

LADY JAYDEE AONDOLEWA KWENYE SAUTI ZA BUSARA

                         Mwanamuziki Lady Jaydee ameondolewa kwenye orodha ya wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza katika tamasha la sauti z... [Read More]

Gari aliyokuwa akitumia James Argent ikiwa imeumia mara baada ya kupata ajali,huku sehemu ya gari ikiwa na mabaki ya manyoya ya mnyama aliyemgonga
James Argent ambaye ni Muigizaji wa Tamhilia ya The Only Way is Essex,amenisurika kufa akiwa safarini kuelekea Jijini London,wakti akiwa njiani akitoka nje kidogo ya jiji hilo ambapo alikuwa na waigizaji wenzie wakitoka kurekodi baadhi ya vipande vya tamthia hiyo..Akihojiwa na Police waliofika kupatia msaada  alisikika  akisema "nilikuwa katika mwendo kasi Ghafla nikaona Mnyama akivuka barabara ndio katika harakati za kumkwepa ndipo nikapoteza mwelekeo...

MUIGIZAJI ARGENT JAMES ANUSURIKA KATIKA AJALI

Gari aliyokuwa akitumia James Argent ikiwa imeumia mara baada ya kupata ajali,huku sehemu ya gari ikiwa na mabaki ya manyoya ya mnyama aliye... [Read More]

Wakati tukiwa tumebakiza masaa machache ili kuumaliza mwaka 2011 Joseph Haule Proffesor Jay amesema changamoto ambayo ni kubwa mpaka sasa kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ni kuwa na msimamo kwani bado wanayumbishwa na washika dau wa muziki wa kizazi kipya.Pamoja na mafanikio makubwa na mapinduzi ya muziki.wasanii tunatakiwa kuwa kitu kimoja na msimamo mmoja..vile vile ameoa ushauri kwa wasanii wenzake wawe wanajiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadae maana wasanii wengi wanapata mafanikio na fedha ila wengi hufilisika kutokana starehe wazifanyazo wakati wa mafanikio ni vizuri kujiwekea akiba

PROFFESOR JAY "WASANII BADO HATUNA MSIMAMO"

Wakati tukiwa tumebakiza masaa machache ili kuumaliza mwaka 2011 Joseph Haule Proffesor Jay amesema changamoto ambayo ni kubwa mpaka sasa kw... [Read More]

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging