Mwanamuziki wa Bongo Flava Barnaba anatarajiwa kuondoka nchini kwenda nchini Ufaransa kwa ajili kurekodi na mwanamuziki Fally Ipupa ambaye awali walikuwa waifanye shughuli hiyo hapa Dar.Barnaba alikaririwa akiosema kuwa amepata ofa ya kurekodi na mwanamuziki Fally Ipupa ikiwa ni takribani miezi miwili tangu deal hiyo iote mbawa baada ya Fally kukatiza ziara yake baada ya fujo zilizotokea huko Arusha.Katika tukio hilo ambalo lilimkasirisha Fally kiasi cha kukatisha ziara yake kutokana na tatizo la umeme ambao ulikuwa ukikatika katika na mashabiki kukasirika na kufanya fujo.
Barnaba amesema kuwa aliwasiliana na meneja wa Fally huko Ufaransa na kukubaliwa kufanya kolabo hiyo bure lakini ajigharamie usafiri ambao alisema unafikia Tanzania Shilingi Milioni nne (4,000,000/-).
Binafsi Barnaba ni mmoja ya wanamuziki ambao ninawakubali sana, naweza sema THT imefanikiwa kutoa vijana wazuri inawezekana kutokana na kupewa airtime ya kutosha lakini nadhani mafunzo wanayopata yanawasaidia sana.