Mwanamuziki Koffi Olomide amefikishwa mahakamani kwa mara nyingine kwa makosa matatu yakiwemo udhalilishaji na kuwabaka wanamuziki wake wa kike.Akiongea na shirika la utangazaji la AFP wakili wa Koffi Bw. Manuel Aeschlimann, Aidha habari zinasema kuwa Olomide alijipeleka mwenyewe kwa Judge siku ya jumatatu huko Nanterre ambako mashtaka hayo yamefunguliwa.
Habari zinasema kuwa Olomide aliondoka kurejea Kongo bila kusubiria hukumu yake kutokana na makosa yaliyotajwa. Pia wakili huyo alisema kuwa Olomide hana la kujibu kwa kuwa wanamuziki hao mashtaka yao hayana ukweli wala ushahidi ndani yake, kisha akaongeza kuwa wanamuziki hao walitaka kupata vibali vya kuishu nchini Ufaransa kwa kumchafulia mteja wake.