Mara baada ya Sumalee kuja na ngoma yake hakunaga kufanya vyema katika soko la muziki ,anatarajiwa kupiga shoo moja Muscat, Oman na nyingine Dubai, Falme za Kiarabu.Mchongo mzima umeelezwa na mkali anayebamba katika Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambaye ameeleza kuwa kwenye shoo hizo watapiga mzigo pamoja.
Diamond akiongea na pro-24 kwa njia ya simu amesema show zilikuwa zifanyike Januari 27, mwaka huu, siku ambayo alitakiwa kuwepo Falme za Kiarabu kwa ajili ya show hiyo..,Alisema, shoo zake za Januari 26 na 27, mwaka huu, zilisogezwa mbele na sasa hatakwenda peke yake, bali ataongozana na Sumalee.“Sijajua nini hasa kilitokea ila waliahirisha shoo na kusogeza mbele. Tutakwenda kufanya makamuzi na nitakuwa na Sumalee kama ambavyo tumekubaliana na waandaaji wa maonesho hayo,” alisema Diamond bila kutaja siku ambayo matamasha hayo yatafanyika.









