Google PlusRSS FeedEmail

NURU NASSOR KATIKA MGOGORO MKUBWA KATIKA NDOA YAKE NA LUQMAN

Ndoa ya staa wa sanaa za maigizo Bongo, Nuru Nassor ‘Nora’ inashikiliwa na nyuzi moja dhaifu kwa sababu yupo kwenye ‘mgogoro’ zito na mume wake, Masoud Ali ‘Luqman’.Habari kuwa Nora na Luqman hapatoshi, zimemiminwa na mtoa habari makini ambaye ameeleza kuwa chanzo ni kauli ya mrembo huyo aliyoitoa hivi karibuni kwenye gazeti moja nchini.
Kauli aliyoitoa Nora kuwa yupo tayari kuomba talaka endapo mume wake hatamruhusu kucheza filamu ndiyo iliyoibua ‘timbwili’ ndani ya familia hiyo yenye wanachama wawili.
“Mume wake aliposoma gazetini kauli ile, moja kwa moja alipitisha uamuzi wa kumuacha mkewe lakini ndugu wameingilia kati kunusuru ndoa hiyo,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:“Hata hivyo, maelewano bado siyo mazuri. Wamesuluhishwa lakini mwanaume bado haelewi. Anasema Nora amemdhalilisha kupita kiasi na anaamaini hana mapenzi naye.”Jitihada za ripota wetu kumpata Luqman ziligonga ukuta lakini Nora alipovutiwa waya hewani, alikiri kuwepo kwa mtafaruku mzito na mume wake.“Naumia sana, sikutegemea kama yale maneno yangemuudhi mume wangu na watu wengine, kwa sasa nipo katika hali ngumu ya kuweka mambo sawa ili nieleweke kwamba sikuwa na nia mbaya.“Watu wananiona kituko, familia yangu hainielewi najuta kwanini nilitoa kauli ile, naomba nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa kila mtu aliyekwazika na kauli niliyoitoa,” alisema Nora.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging