Si mwingine bali ni yule Mwigizaji anayechipukia kwa kasi Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameamua kuyaanika maisha yake kupitia Filamu yake ya kwanza itwayo ‘Foolish Age’, inayotarajiwa kuingia sokoni siku za usoni kuanzia sasa.Lulu alisema ndani ya Filamu hiyo pia atatumia jina la Lulu, na kwa kiasi kikubwa itazungumzia sehemu ya maisha yake.Mbali na hilo alisema kuna vitu vingi amevipata kwenye maisha ya ukweli, ambavyo vitaonekana kwenye hiyo ‘Filamu’.Alisema kama vile wakati akitoroka nyumbani kwenda disko, na kuwa kwenye makundi yasiyo mazuri.Katika Filamu hiyo amewashirikisha wasanii mbalimbali wenye majina, miongoni mwao wakiwa Mboto na Hasheem Kambi na kwamba mashabiki wasubiri vitu vyake.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








