Google PlusRSS FeedEmail
Showing posts with label MOVIE. Show all posts
Showing posts with label MOVIE. Show all posts
              
Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere amesema Juni 6 mwaka huu wanatarajia kuzindua Tuzo za kwanza za Bongo Movie,
Steve nyerere amesema tayari wameshatafuta wadau kwa ajili ya kufanikisha tuzo hizo
Alisema kwa sasa wapo kwenye mikakati ya mwisho kuhakikisha wanapata mgeni rasmi atakayezindua kwa mara ya kwanza tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kuzinduliwa katika Hotel  ya Serena Jijini Dar es salaam

TUZO ZA BONGO MOVIE KUZINDULIWA JUNE 6

               Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere amesema Juni 6 mwaka huu wanatarajia kuzindua Tuzo za kwanza za Bongo Movie, Steve... [Read More]


Serikali kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya iitwayo scola vinginevyo haitaruhusiwa kuingia mtaani.

taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za kitanzania, imeeleza kuwa aunt aliipeleka filamu hiyo ili ikakaguliwe kama zilivyo taratibu lakini bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya maadili ya mtanzania.

“kuna vipande vitatu ambavyo kimsingi vimevuka matakwa ya maadili ya kitanzania hivyo hakuna jinsi, lazima avitoe kama anataka kuiingiza sokoni sinema hiyo,” kilieleza chanzo makini ndani ya bodi hiyo kilichoomba hifadhi ya jina.


kabla ya mwandishi wetu hajazungumza na aunt, alimpata rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa rafiki yake (aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee.


“amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie mtaani pasipo kuviondoa hivyo vipande kwani navyo vina umuhimu wake,” alisema rafiki huyo wa aunt kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.

alipotafutwa aunt kuhusiana na suala hilo, alikiri kukaliwa kooni na bodi na kuomba apewe muda wa siku mbili ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hilo lakini hakufanya hivyo, badala yake akasafiri nje ya nchi.



mwaka jana mwishoni, bodi hiyo ya filamu ilimzuia mwigizaji vincent kigosi ‘ray’ kuingiza sokoni sinema ya sister mary baada ya kuridhishwa na madai ya kanisa katoliki yalioainisha kuwa asilimia kubwa vipande vya sinema hiyo vilidhalilisha ukatoliki.

FILAMU YA AUNT EZEKIEL YAZUILIWA BAADA YA KUWA NA VIPANDE VYENYE KUCHOCHEA NGONO

Serikali kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya i... [Read More]

KATIKA hali ya kushangazwa na kuonyesha jinsi gani mwanadada nyota katika tasnia ya filamu Jacqueline Wolper ni kivutio, wanafunzi wa shule ya msingi Baracks ilipo maeneo ya Kilwa Road walitimkia nje kwa ajili ya kwenda kumwona Jack huku wengine wakimrukia mwilini mwake na kumfanya awe katika wakati mgumu hadi Polisi walipokuja na kuwaamuru wanafunzi hawa kurudi madarasani walikokuwa wamewakimbia walimu wao.Jack alifika katika maeneo hayo kwa ajili ya kukagua maeneo kwa ajili ya kurekodia filamu mpya ya Injinia iliyoandikwa na msanii wa filamu na vichekesho Issa Kipemba ‘Kipemba’ Jack alikuwa ni mmoja kati ya majaji waliofanya usaili katika usaili uliofanyika Kilwa Road sehemu ya Polisi Bendi.“Nimefurahia sana kwa kupokelewa na wanafunzi kwa hamasa kama hiyo pamoja kuwa walikuwa wanataka kunizidi nguvu lakini nimefurahi nao kwani hawa ndio wapenzi wetu wa kazi za filamu, tunafurahi tunavyoona wanatukubali katika maeneo tunayofanyia kazi ni ushindi katika tasnia ya filamu,”anasema Jack.
Pia msanii huyo ni mmoja kati ya wasanii watakaoshiriki katika filamu hiyo ya Injinia filamu inayotabiriwa kutengenezwa kitaalamu zaidi kufuatia mtunzi wa filamu hiyo kujikita katika utafiti na kutumia wanataluma katika masuala ya upelelezi, filamu hiyo itarekodiwa na kampuni ya Papa zi ya jijini Dar es Salaam..

JACK WOLPER AWAPAGAWISHA WANAFUNZI

KATIKA hali ya kushangazwa na kuonyesha jinsi gani mwanadada nyota katika tasnia ya filamu Jacqueline Wolper ni kivutio, wanafunzi wa sh... [Read More]

Mtayarishaji wa filamu  Chrissent Mhenga  amesema kuwa tasnia ya filamu inahitaji mabadiliko makubwa ili ilete tija na maslahi kwa watayarishaji na wasanii kwa ujumla, Chriss ameyasema hayo wakati akijiandaa kuandaa filamu mpya inayotarajia kuwashirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu Chriss ambaye ndiye mwasisi wa kizazi kinachotamba katika filamu ameamua kuingia rasmi katika filamu. “Ukweli haupingiki kuwa wasanii wote nyote wametoka katika kundi la Kaole ambalo mimi nilikuwa Mkurugenzi wake, na niliweza kuwajenga na wameweza kuliteka soko la tasnia ya filamu hivi sasa lakini kuna jambo moja tu ambalo naliona ni matatizo ya hadithi hazishiki watu kwa muda mrefu tofauti na awali nilipokuwa nikiandikia wasanii hawa katika kundi la Kaole Sanaa Group,”anasema Uncle Chriss. Muongozaji huyo wa filamu hapa nchini ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya Mega Video amekusudia kuanza kurekodi filamu mpya baada ya filamu yake ya kwanza ya Hazina ya Marehemu kufanya vizuri na kupata maoni mengi kutoka kwa wadau wengi, lakini anawasisitizia wasanii kujitahidi kujifunza vitu vya kitaaluma kwani hata filamu nyingi zimekuwa zikikosa uhalisi kwa kukosa taarifa kwa wahusika. 

FILAMU INAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA

Mtayarishaji wa filamu  Chrissent Mhenga  amesema kuwa tasnia ya filamu inahitaji mabadiliko makubwa ili ilete tija na maslahi kwa watay... [Read More]

Jaqueline Wolper Massawe ‘Jack’ anasema kuwa suala la mavazi mara nyingi utegemea tukio au sehemu husika tofauti na watu wanavyofikiria kuwa unapomwona msanii huyo katika mavazi fulani ndio wanajua ni mavazi yake halisi, na kulalamika kama wasanii ndio wanaovaa vibaya katika jamii   Mara nyingi mavazi yanategemea sana sehemu husika hata nikiwa (Star) Nyota siwezi labda kwenda kanisa nimevaa kimini na sehemu ambazo hazistaili kwa mavazi yaliyo tofauti bali nitavaa vazi linalostahili, lakini kwa bahati mbaya lawama inatuangukia sisi wasanii tukionekana kama ndio tunaovaa vibaya,”anasema Jack.
Aidha amesema kuwa inakuwa vigumu mtu ukienda sehemu kama Disco hauwezi kuvaa sehemu nyingine isiyohusika, lakini pia amesema kuwa kuna nguo zinavaliwa katika filamu tu na mtu hawezi kuvaa mtaani, pamoja na kuwaangalia sana wasanii lakini pia wasanii nao ni sehemu ya jamii jambo ambalo inatakiwa pia watu walione hilo kwani kuna watu si wasanii na wana viwalo vya ajabu...

JACK WOLPER "SI WASANII PEKEE WANAOVAA BIBAYA "

Jaqueline Wolper Massawe ‘Jack’ anasema kuwa suala la mavazi mara nyingi utegemea tukio au sehemu husika tofauti na watu wanavyofikiria k... [Read More]

Zaidi ya wasanii 500 wamejitokeza katika usaili kwa ajili ya kushiriki katika maandalizi ya filamu fupi fupi zitakazojulikana kwa jina la Kiduchu Films, usahili huo ulifanyika leo hii katika viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni na kuhudhuriwa na umati wa watu mbalimbali huku wote wakiwa na shauku ya kuibuka kama washindi watakaochaguliwa, mratibu wa zoezi hilo Nkwabi Juma amesema..,“Tunashukru kwa wananchi kuitikia mwito kwa kuja kushiriki katika usaili kwa siku ya leo japo ni siku ya mapumziko lakini mwitikio umekuwa mkubwa sana, na kama laiti watu wote wangefika mapema kwa muda tuliotangaza sehemu kubwa ya zoezi ingefanyika kwa wakati na tukio hili kumalizika, sasa mchana ndio watu wanazidi kumiminika,”amesema Nkwabi. Katika usahili huo watu waliokuwa wanahitajika ni Waongozaji wa filamu, Wasanii, Waandishi wa muswada na wapiga picha, baada ya usaili wahusika watafundishwa kitaalamu jinsi ya kufanya kazi hizo kisha kukabidhiwa jukumu la kurekodi filamu hizo

ZAIDI YA WATU 500 WAJITOKEZA KATIKA KIDUCHU FILMS.

Zaidi ya wasanii 500 wamejitokeza katika usaili kwa ajili ya kushiriki katika maandalizi ya filamu fupi fupi zitakazojulikana kwa jina l... [Read More]

SERIKALI imetekeleza ahadi iliyotoa wakati wa msiba wa gwiji la tasnia ya filamu  Marehemu Steven Kanumba, zoezi hilo lilifanyika nyumbani kwa marehemu Kanumba Sinza Vatcan City, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Amos Makalla aliwakilisha serikali kutoa rambirambi ya shilingi milioni 10, kwa familia ya Marehemu Kanumba.Pamoja na kutoa rambirambi, Naibu Waziri Makalla alisisitiza kuwa kifo cha Kanumba kimeleta chachu na kuahidi kuwa serikali itajikita kikamilifu kusimamia kuboresha pato la wasanii wote ikiwa wasanii wa filamu ambao mara nyingi jamii imekuwa ikiwaona kama ni watu wenye maisha ya kitajiri kumbe ni tofauti na ukweli halisi. Mama yake na marehemu Kanumba akiwa na fedha alizopokea kutoka kwa Serikalini pichani kulia ni Naibu waziri Mh. A.Makala.
“Serikali imejifunza kupitia kifo cha Msanii wetu aliyelitangaza Taifa kwa kazi zake lakini hajafaidi kabisa jasho lake kutokana na wizi wa kazi zao, serikali inapanga mipango itakayotoa fursa kwa wasanii kufaidika na kazi zao,”alisema Mh. Makala.Naye mama wa Marehemu ameishukru Serikali kwa kumuunga mkono katika kipindi kigumu cha msiba mwanaye kwani amepata changamoto nyingi kutoka kwa mzazi mwenzake huku hata jamii ikijaribu kuamini kuwa marehemu Kanumba alikuwa na mali nyingi kulingana na kazi alizofanya kumbe hakuwa na fedha hizo zinzohisiwa.“Kweli inakatisha tamaa sana mwanagu kaigiza filamu 42 lakini kama kuanza kujitegemea ameanza mwaka 2010 tu, maisha yake yote alikuwa akiishai kwangu kupanga hata miaka miwili hajamaliza ina maana angefika mwezi wa saba ndio ingekuwa miaka miwili Naishukru sana Serikali kwa kunisaidia kwa kila hatua,” anasema mama Kanumba.

MH. MAKALA ATOA RAMBIRAMBI KWA KANUMBA

                               SERIKALI imetekeleza ahadi iliyotoa wakati wa msiba wa gwiji la tasnia ya filamu  Marehemu Steven Kanumba... [Read More]


MWIGIZAJI Chipukizi katika tasnia ya filamu  Sadikina Mussa anasema kuwa katika tasnia ya filamu hana mpinzani kabisa angalau kidogo mtu ambaye anaweza kwenda naye sambamba na kumfikia katika uigizaji kwa wasanii wa kike ni Wema Sepetu tu ndio anayemuona anaweza kushindana naye katika fani hiyo ya uigizaji. “Sioni kama kuna msanii wa kike mwenye uwezo wa kuigiza kama mimi katika tasnia ya filamu kwa sasa, kwani wasanii wengi mara nyingi wapo vile vile hawabadiliki, mpinzani tena kidogo labda anaweza kuwa Wema Sepetu, Wema uigizaji wake ni wa uhalisia kama sura ninayo pia mvuto ninao na najua kuigiza,”anasema Sadikina.Msanii huyo ambaye ameshiriki katika filamu kadhaa hivi sasa anakuja na filamu ya Harakati kutoka kampuni ya SSG Distributors, msanii huyo ambaye amefanana kimuonekano kama Wema Sepetu ni kipaji kilichovumbuliwa na Mshindo Jumanne, katika filamu ya Harakati ameigiza kama mhusika mkuu...

SADIKINA MUSSA MPINZANI WA WEMA SEPETU

MWIGIZAJI Chipukizi katika tasnia ya filamu  Sadikina Mussa anasema kuwa katika tasnia ya filamu hana mpinzani kabisa angalau kidogo mtu a... [Read More]

Mwigizaji Nyota anayekuja juu katika tasnia ya filamu Nchini Elia Daniel ‘Allen’ anasema kuwa filamu yao mpya ya Blood House (Nyumba ya Damu) inayotarajia kuingia sokoni hivi karibuni kwake imeleta faida kubwa kutokana na kufanya kuweza kumpata mchumba ambaye ni Anna Matee aliyeigiza kama Angel, katika filamu hiyo Allen na Angel wameigiza kama mke na mume“Filamu hii ya Blood House ni filamu ya kipekee sana na ni kazi ambazo kwangu mimi ni fahari kwa kuniletea faida kubwa nyingi tu, ikiwa ni pamoja na kuwa na mpenzi wa kweli ambaye ni Angel niliyecheza naye kama mke wangu katika filamu hiyo lakini pia kwa sasa ni mchumba wangu na mungu akipenda tunaweza kuwa kweli ni mke na mume kama ilivyokuwa katika Blood House,”anasema Allen 
Allen ni msanii ambaye mbali na kuigiza pia ni muongozaji wa filamu ameshiriki katika filamu kama God is Great, Damu ya Mjomba, Im not my Brother, Maisha ya siri, Gamba la nje Hellen, katika filamu ya Blood House imeshirikisha wasanii nyota kama Mohamed Fungafunga ‘Mzee Jengua’, Charles Magali ‘Mzee Magali’, Chuchu Hans, Anna Matee ‘Angel’, Elia Daniel ‘Allen’ msanii huyo anasema kuwa filamu hiyo si ya kuikosa kutokana na kiwango chake...

KWA HISANI YA FC

BLOOD HOUSE IMENIPA MCHUMBA- ALLEN

Mwigizaji Nyota anayekuja juu katika tasnia ya filamu Nchini Elia Daniel ‘Allen’ anasema kuwa filamu yao mpya ya Blood House (Nyumba ya ... [Read More]

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu  Nchini  Emanuel Myamba  Pastor Myamba yupo katika sehemu mbalimbali akimalizia kurekodi filamu yake mpya inayoitwa Gods Kingdom ikiwa ni majibu ya filamu iliyoigizwa na marehemu Steven Kanumba ya Devil Kingdom akiongea Pastor Myamba anasema filamu hiyo inakuja kuonyesha uwezo wa Mungu.“Filamu ya Gods Kingdom ni majibu ya filamu ya Devil Kingdom iliyoigizwa na marehemu rafiki yangu Kanumba, katika filamu yake alionyesha jinsi gani nguvu za giza zinavyofanya kazi, lakini katika filamu ya Gods Kingdom unaona uwepo wa Mungu na akijibu maombi kwa kila amwombaye, ni filamu ya kipekee kabisa,”anasema Pastor Myamba.Filamu hiyo ya Gods Kingdom ipo katika hatua za mwisho katika kurekodiwa kinara wa filamu hiyo ni Pastor Myamba mwenyewe, wasanii wengine ni Zawadi, Elizabeth Chijumba ‘Nikita’, Mzee Maneto, Pacho Mwamba wanafunzi wa TFTC wanaosoma katika chuo hicho mafunzo ya uigizaji na utengenezaji wa filamu..

PASTOR MYAMBA AMJIBU KANUMBA

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu  Nchini  Emanuel Myamba  Pastor Myamba yupo katika sehemu mbalimbali akimalizia kurekodi filamu yake... [Read More]

Mara baada ya msanii wa filamu nchini Sajuki kuanza kuchangiwa pesa ya matibabu na wapenzi wa tansia ya filamu nchni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Jacqueline wolper ameguswa na kutoa mchango kwa ajili ya matibabu ya msanii mwenzake Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Jack ametoa Dola 10,000/ kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo anatakiwa kwenda kutibiwa nchini India baada ya kwenda mara ya kwanza na kutakiwa tena kurudi kwa ajili ya matibabu zaidi.Nimeguswa sana na tatizo lake si kwamba nina fedha nyingi na sina shida, bali ni moyo wa kusaidia kuokoa uhai wa mwenzetu ili atibiwe nakurudi katika shughuli zake za filamu, Tulizoea kuwa naye location na kwenye tasnia ya filamu kwa ujumla, na sasa anaumwa na hajiwezi, nimeumia sana,”alisema Jack.
Pro-24 kumpongeza mwanadada huyu mwenye moyo kujitolea kutoka moyoni kwani tunaamini kabisa fedha kama hiyo angeweza kuitumia kwa matumizi yoyote lakini ameamua kusaidia matibabu ya ndugu yetu Sajuki Mungu amtie nguvu na kupata fedha nyingi zaidi hizo kutoa ni moyo wala si utajiri.

JACK WOLPER AMCHANGIA SAJUKI DOLA 10,000.

Mara baada ya msanii wa filamu nchini Sajuki kuanza kuchangiwa pesa ya matibabu na wapenzi wa tansia ya filamu nchni mwigizaji na mtayar... [Read More]


Aliweza kutoa shinikizo hilo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, muda mfupi baada ya wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU), Leonard Swai, kuikumbukusha mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja jana kwa ajili ya upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao, lakini akadai hilo halitaweza kufanyika, kwa sababu hajaja na mashahidi na anaomba kesi hiyo iahirishwe.

Kwani kesi hiyo humkabili msanii wa Filamu hapa nchini, Kajala Masanja na siku chache zilizopita aliweza kumwaga machozi huku akiujia juu upande wa Jamhuri kwenye kesi inayomkabili ya usafishaji fedha haramu ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hapa Jijini.Baada ya wakili huyo kumaliza kutoa maelezo hayo, ndipo Kajala akanyosha kidole na kuomba ruhusa ya mahakama ili aweze kuzungumza jambo.
Msanii huyo alipata mwanya wa kuongea na Mheshimiwa Hakimu huku akibubujikwana machozi na kusema kwamba, "Hivi huyu wakili wa serikali anafikiri kule Segerea ninakoishi kwa sasa ni sehemu ya starehe? Mahabusu kunatisha, wewe wakili wa serikali lete mashahidi kesi isikilizwe,”Mbali na hilo Hakimu Fimbo aliwezakuhairisha kesi hiyo hadi kufikia Mei 9, ambapo upande wa jamhuri unatakiwa ulete mashahidi wake ili waanze kutoa ushahidi.
Ilidaiwa na Wakili Swai kwamba Machi 27 mwaka huu mbali na mshitakiwa Kajala...mshitakiwa mwingine ni mumewe Faraja Chambo, wanakabiliwa namakosa matatu.Alisema kosa la kwanza linalowakabili washitakiwa hao ni pamoja na kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa ya mwaka 2007, ambapo wote wawili walitenda kosa hilo la kula njama la kuhamisha umiliki wa nyumba iliyoko Kunduchi Salasala eneo ambalo halijapimwa hapa Jijini.Kosa la pili ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010, walihamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo, ambayo walikuwa wakiimiliki kwenda kwa Emilian Rugalia, ambaye ndiye waliyemuuzia kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya TAKUKURU ya mwaka 2007. Na shtaka la tatu ni la kutakatisha fedha, ambalo walilitenda siku hiyo ya Aprili 14, 2010 huku wakijiua ni kinyume cha sheria hiyo.Mshitakiwa Chambo naye yuko mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, kwa sababu anakabiliwa na kesi nyingine ya utakatishaji fedha haramu, iliyofunguliwa mahakamani hapo, ambapo kwa mujibu wa sheria, kosa hilo halina dhamana.

"KAJALA"MH HAKIMU SEGEREA KUNATISHA SANA

Aliweza kutoa shinikizo hilo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, muda mfupi baada ya wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (T... [Read More]

Mwigizaji na Mtayarishaji wa filamu Nchini Issa Mussa ‘Cloud" yupo katika maandalizi ya kuzindua filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Toba uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Salama uliopo Zanzibar tarehe 18/05/2012 siku ya Ijumaa.Cloud anakuwa ni msanii wa kwanza kwa mwaka huu kufanya tamasha kwa ajili ya uzinduzi wa filamu yake hiyo ya Toba baada ya utaratibu huo kusimama kwa muda mrefu kidogo, kwani siku hizi filamu zikitengenezwa zinaingizwa sokoni moja kwa moja bila kufanyiwa uzinduzi.Filamu ya Toba imeshirikisha wasanii nyota kama Suleiman Barafu, chiki, Sandra, Eshe, Bi. Hindu na wasanii wengine wakali katika tasnia ya filamu nchini... 

CLOUD KATIKA HARAKATI ZA UZINDUZI WA TOBA

Mwigizaji na Mtayarishaji wa filamu Nchini Issa Mussa ‘Cloud" yupo katika maandalizi ya kuzindua filamu yake mpya inayokwenda kwa ji... [Read More]

Bastola ambayo inadaiwa ilikuwa ikitumiwa kihalali na staa wa filamu barani Afrika, Steven Charles Kanumba, inasakwa na Jeshi la Polisi Tanzania.Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Charles Kenyela amesema kuwa anafuatilia kumbukumbu za silaha hiyo, kwani haijarejeshwa kwenye jeshi lake.Kenyela alisema juzi kuwa anafuatilia umiliki wa Kanumba juu ya umiliki huo na baada ya hapo, jeshi la polisi litawahoji ndugu“Bastola ni mali ya serikali. Kuna hatua ambazo hufuata mpaka mtu aruhusiwe kumiliki bastola,” alisema Kenyela na kuongeza:Endapo mmiliki halali wa silaha hiyo atafariki dunia, ndugu zake lazima waikabidhi kwa jeshi la polisi na baada ya hapo, kama kuna ndugu anataka aimiliki, inabidi afanye maombi upya na atakapokidhi vigezo ndiyo anaruhusiwa.“Kutokana na hali hiyo, bastola ya Kanumba lazima irudi kwetu haraka na kama kuna ndugu yake yeyote anataka kuimiliki, itabidi awasilishe maombi.”Kenyela aliongeza kuwa hivi sasa anafuatilia kumbukumbu za jeshi la polisi ili awe na uhakika kama kweli msanii huyo alikuwa anamiliki silaha hiyo.“Tukithibitisha tutawahoji ndugu zake pamoja na wengine wanaohusika ili tuwe na taarifa za hiyo silaha. Ila kwa sasa tunafanyia kazi taarifa hizi kwa kupitia kumbukumbu za jeshi,” alisema.Kenyela alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa na ripota wetu kama jeshi lake limeshapokea bastola ambayo alikuwa anaitumia Kanumba enzi za uhai wake.
NDUGU WANASEMAJE?
Mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa, aliulizwa na paparazi wetu kuhusu bastola inayodaiwa kutumiwa na mwanaye alipokuwa hai, na haya ni majibu yake:“Sijaiona hiyo bastola humu ndani tangu nimefika hapa. Sijui ipo wapi na sijui kama kweli Kanumba alikuwa anamiliki hiyo silaha.“Najua sheria za silaha hiyo, kwa hiyo ingekuwepo ningeiwasilisha polisi haraka. Baba yangu alikuwa na silaha hiyo, alipofariki dunia tuliikabidhi kwa jeshi la polisi.”
NANI ANAJUA ILIPO?
Taarifa zinaonesha kuwa mdogo wa Kanumba, Seth Bosco alikuwa karibu zaidi na marehemu lakini kwa sababu umiliki wa silaha hiyo ni siri, siyo rahisi kujua ilipo.Mtu mwingine ambaye alikuwa karibu na marehemu mpaka nyakati za mwisho za uhai wake, kama ripoti zinavyoonesha ni muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, ingawa naye inawezekana akawa hajui kutokana na unyeti wa silaha yenyewe.
BASTOLA NA KANUMBA
Akiwa hai, Kanumba aliwahi kuripotiwa mara kadhaa kumiliki silaha hiyo, japo haikufafanuliwa kama ni kihalali au batili.Kanumba aliripotiwa kwa mara ya kwanza kumiliki bastola miaka minne iliyopita, akidaiwa kuichomoa baada ya kuvamiwa na kundi la watu aliohisi wanataka kumteka.Licha ya stori hiyo kuandikwa gazetini na nyingine ambazo zilimhusisha na umiliki wa bastola, bado Kanumba hakuwahi kufafanua chochote kuhusu silaha hiyo.
IPO WAPI?
1. Je, aliiacha sehemu ambayo hakuna mtu ameweza kupafikia?
2. Aliirejesha kabla mauti hayajamkuta ndiyo maana haionekani?
3. Je, Kuna mtu aliiwahi baada ya kifo chake akiona ni dili?
Kanumba alifariki dunia Aprili 7 na kuzikwa Aprili 10, 2012 kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. wa msanii huyo kuhusu kurejesha bastola hiyo jeshini.

KENYELA AMESEMA ANAFUATILIA BASTOLA ILIYOKUWA IKIMILIKIWA NA KANUMBA

Bastola ambayo inadaiwa ilikuwa ikitumiwa kihalali na staa wa filamu barani Afrika, Steven Charles Kanumba, inasakwa na Jeshi la Polisi T... [Read More]

Tangu jana kitaani na kwenye mitandao ya kijamii kumekuwepo na rumors juu ya kifo cha muigizaji na Director wa filamu Sajuk , Kutokana na taarifa hiyo lawama zote zikamuangukia Actor ambaye pia
ni mwimbaji wa Bongo Flava Hemedy  ambaye inadaiwa ndiye aliyeandika taarifa hizo kwa mara ya kwanza katika status yake ya facebook kuwa Sajuk  ameaga dunia..  Hemedy  amesema yeye hausiki kabisa nakuandika taarifa hizo ila kuna mtu amefungua ukurasa katika mtandao wa   facebook kwa jina  la Hemedy na kuandika ujinga huo ila nini kauli ya Sajuk "napenda kuwaambia mashabiki wangu ni kweli naumwa ila kwa sasa hali si mbaya sana naendelea vyema na kwa sasa niko location nafanya filamu yangu mpya .niliposikia habari kwamba nimekufa kweli zimenishtua sana ila napenda kuwaambia maadui zangu kwamba kama mwenyezi Mungu akipenda na wakati utakapofika atachukua uhai wangu ila sitakufa kwa maneno yao,"Wapenzi wangu kaeni mkao wa kula maana filamu yangu mpya iko njiani  alimazia Sajuki  "Nae mke wa sajuki alikuwa na haya ya kusema "Ninaomba wadau wa filamu pamoja na Watanzania wote kutuchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya Sajuki mume wangu ambaye ni mhimili mkubwa katika familia yetu na jamii nzima kwa ujumla fedha inayohitajika ni nyingi sana, mchango wako ni muhimu sana tunatanguliza shukrani zetu kwenu nyote mnayeguswa na tatizo hili,Kwa wale wanaoguswa na msanii huyu tunaomba wachangie michango hiyo kwa kupitia Tigo – Pesa kwa namba 0713 666 113 Wastara Juma pia unaweza kutama fedha hiyo kwa kutumia Akaunti namba 050000003047 Akiba Commercial Bank.

KAULI YA SAJUK MARA BAADA YA KUZUSHIWA KIFO..

Tangu jana kitaani na kwenye mitandao ya kijamii kumekuwepo na rumors juu ya kifo cha muigizaji na Director wa filamu Sajuk , Kutokana n... [Read More]

Mwigizaji wa filamu katika tasnia ya filamu  Devotha Mbaga amebainisha kuwa pamoja na
watayarishaji kujitahidi kutengeneza filamu katika ubora mkubwa tatizo kubwa linalowakabili ni kukosa makampuni ya usambazaji wa filamu hizo, jambo linalosababisha wajikute wakiwa katika foleni kwa muda mrefu.“Tatizo kubwa ni usambazaji wa filamu kwa sasa, kwani msambazaji anayelipa vizuri ni mmoja tu ambaye ndiye mkubwa na kuna wasanii anaowamiliki kwa maana ya kuwa na mikataba nao, wasanii wenye mikataba hawana shida ya kukaa foleni, wasambazaji wadogo wapo lakini wananunua kazi kwa bei ya chini sana jambo ambalo hauwezi hata kurudisha gharama za utengenezaji wa filamu yenyewe,”anasema Devotha.
Msanii huyu ambaye anamiliki kampuni yake ya Jaber Entertainment anasema kuwa kuna wakati watayarishaji wanajikuta wakisubiri majibu kutoka kwa msambazaji zaidi ya miezi hata sita jambo linalowatesa kwani wanakaa muda mrefu kwa filamu moja tu, anaiomba Serikali kuwekeza katika filamu kwa kuweka kampuni nyingine za usambazaji. Filamu alizotayarisha na kuigiza ni Bora nife na filamu ya Cross of Love.

USAMBAZAJI FILAMU KIKWANZO NCHINI

Mwigizaji wa filamu katika tasnia ya filamu  Devotha Mbaga amebainisha kuwa pamoja na watayarishaji kujitahidi kutengeneza filamu kati... [Read More]

Nyota katika tasnia ya filamu Nuru Nassor ‘Nora’ baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu katika mambo ya uigizaji wa filamu amerudi tena kwa nguvu zote kwa kuingia na filamu inayojulikana kwa jina la I Can’t Forgive, filamu hiyo ipo sokoni na inakimbiza filamu za wakongwe wanaofanya vizuri.Watayarishaji ambaye hakutaka jina lake litajwe katika habari amesema kuwa msanii huyo kuwa ni msanii mwenye uwezo wa hali ya juu sana na kwa upande mwingine ndiye kabeba sehemu kubwa ya filamu hiyo na kuifanya iwe ni ya kipekee zaidi. Mmoja wa watayarishaji ambaye hakutaka jina lake litajwe katika habari amesema kuwa msanii huyo kuwa ni msanii mwenye uwezo wa hali ya juu sana na kwa upande mwingine ndiye kabeba sehemu kubwa ya filamu hiyo na kuifanya iwe ni ya kipekee zaidi...

NORA KURUDI KWA NGUVU NA I CAN’T FORGIVE.

Nyota katika tasnia ya filamu Nuru Nassor ‘Nora’ baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu katika mambo ya uigizaji wa filamu amerudi tena kwa... [Read More]

Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Nuru Nassor ‘Nora’ baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu katika mambo ya uigizaji wa filamu amerudi tena kwa nguvu zote kwa kuingia na filamu inayojulikana kwa jina la I Can’t Forgive, filamu hiyo ipo sokoni na inakimbiza filamu za wakongwe wanaofanya vizuri mmoja wa watayarishaji ambaye hakutaka jina lake litajwe katika habari amesema kuwa msanii huyo kuwa ni msanii mwenye uwezo wa hali ya juu sana na kwa upande mwingine ndiye kabeba sehemu kubwa ya filamu hiyo na kuifanya iwe ni ya kipekee zaidi“Msanii kama Nora ni wa kiwango cha juu sana iwapo anatumika vizuri katika filamu ya I Can’t Forgive kaitendea haki ameigiza kwa kiwango kikubwa sana ni vema tu wadau wasubiri kazi hiyo nakujionea wenyewe jinsi wasanii walioshiriki katika filamu hiyo walivyoonyesha uwezo wao katika kuigiza,”anasema mtayarishaji huyo

NORA KURUDI KWA NGUVU NA I CAN’T FORGIVE.

Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Nuru Nassor ‘Nora’ baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu katika mambo ya uigizaji wa filamu amer... [Read More]

Muongozaji wa filamu katika tasnia ya filamu Single Mtambalike ‘Richie’ amesema filamu ya Diana ni fundisho kwa wanaume wote wanopenda kuvamia wanawake wa nje huku wakiwa na familia zao, jambo ambalo uleta mitihani katika Ndoa na kuharibu uhusiano katika familia.“Filamu ya Diana ni kipimo cha Ndoa filamu inaonyesha jinsi matatizo ambayo yanaweza kukumba kwa kuwa na Nyumba ndogo na kusalitiwa na kukuteketeza kwa njia ya ushirikina, ukiangalia filamu hii utaona mimi nilivyopoteza kazi na mke wangu kurongwa na Kimada na kupoteza mwelekeo Diana ni kipimo cha Ndoa bora,anasema Richie.
Filamu hiyo imeongozwa na Richie huku akiigiza kama mume wa Ketty ambaye ndio aliyerogwa na Davina na kupooza viungo ni filamu nzuri ina vitu vya kujifunza katika jamii yetu, katika filamu hiyo wasanii walioshiriki ni Subira Rupia, Halima Yahaya, Kupa, Chiki Mchoma, Single Mtambalike na wasanii wengine wakali, unga mkono kwa kununua filamu za wasanii Bongo..




KWA HISANI YA FC

DIANA NI KIPIMO CHA NDOA BORA- RICHIE

Muongozaji wa filamu katika tasnia ya filamu Single Mtambalike ‘Richie’ amesema filamu ya Diana ni fundisho kwa wanaume wote wanopenda ... [Read More]

Muigizaji na Mkali wa ngoma ya kush the man himself rafiki wa karibu na Tupac those days, yuko njiani kufanya filamu ya kutisha iliyopewa jina la “Thaw”.Movie itaandikwa na mkali wa kuandika movies Vick Weet, Kutoka Variety habari zinasema Dr. Dre ataifanya filamu hiyo na rafiki yake Daniel Schnider ambae ndo ameleta wazo hilo. Movie itahusisha mashetani ambayo yatakua yanatokea kwenye barafu inayoyeyuka huko Yukon...Dr Dre sio mgeni Hollywood, The Super Producer/ Rapper alizindua filamu mwaka 2007 na deal ya New Line. Hii ni alama ya toleo la kwanza akiwa chini ya ushirikiano.

DR. DRE KUTENGENEZA MOVIE LA KUTISHA

Muigizaji na Mkali wa ngoma ya kush the man himself rafiki wa karibu na Tupac those days, yuko njiani kufanya filamu ya kutisha iliyopew... [Read More]

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging