Google PlusRSS FeedEmail

NELLY AFANYIWA UPASUAJI WA MGUU.

Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Kimlola A. Kimlola ‘Nelly Kim’ hivi karibuni alifanyiwa upasuaji kwa ajili ya maumivu ya mguu ambayo yalitokana na uvimbe ulioljitokeza katika mguu wake wa kulia, upasuaji huo ulifanyika katika Hospitali ya Regency Kisutu Dar es Salaam kwa sasa msanii huyo hali yake inaendelea vema na yupo tayari kwa ajili ya kazi yake ya uigizaji.
Kim anasema kuwa anamshukru Mungu kwa kumponya na yupo katika mchakato wa kumalizia filamu ya Siyawezi iliyotengenezwa na kampuni ya Take 2 Production ya Jijini Dar es salaam, ipo katika hatua za mwisho ni filamu ya kipekee kwani filamu hiyo imeandaliwa zaidi ya miaka 6. “Namshukru Mungu kwa kuniwezesha kupata matibabu na kupona kwa haraka kwani wakati ugonjwa unaanza kwangu ilikuwa ni mtihani kwa sababu uvimbe wenyewe ulianza kidogo kidogo lakini baadae maumivu yalikuwa makali lakini hivi sasa hakuna tena maumivu baaada ya kutibiwa nawashukru pia madaktari wangu waliofanikisha matibabu haya,”anasema Nelly Kim.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging