ALIYEKUWA mwanamuziki nyota wa muziki wa pop Whitney Houston jana ameagwa ramsi katika kanisa ambalo akiwa mdogo ndipo alianza kuimba la Newark jijini New Jersey, Marekani. Katika shughuli hiyo ya kumuaga mwanamuziki huyo ambayo ilihudhuriwa na marafiki wa karibu pamoja na familia wanamuziki na watu mbalimbali mashuhuri walikuwepo kuhudhuria wakiwemo wanamuziki Robert Kelly, Alicia Keys na Stevie Wonder ambao waliimba katika shughuli hiyo. Watu wengine mashuhuri waliokuwepo ni pamoja na mchungaji na mwanaharakati Jesse Jackson, Kevin Costner ambaye walicheza pamoja katika filamu marufu ya Bordyguard pamoja na mpwa wake Dionne Warwick pamoja na Clive Davis ambaye alikuwa msimamizi wa shughuli zake kimuziki. Mama wa ubatizo wa Whitney Aretha Franklin alishindwa kuhudhuria shughuli hiyo kutokana na hali yake kiafya kutokuwa sawa lakini katika isiyo ya kawaida aliyekuwa mtalaka wa mwanamuziki huyo Bobby Brown aliondoka katika mazishi hayo muda mfupi baada ya kuingia kanisani hapo. Brown aliondoka kanisani hapo kwa kile kinachodaiwa kuingia na watu wengi kanisani ambapo alikuja na timu ya watu tisa wakati katika mwaliko aliopewa aliruhusiwa kuja na watu wawili tu hali iliyopelekea familia ya Whitney kutokubaliana na hivyo kuondoka. Mwili wa mwanamuziki huyo ambaye alikutwa amekufa katika chumba cha hoteli aliyofikia ya Barvely Hilton mwishoni mwa wiki iliyopita na anatarajiwa kuzikwa leo pembeni mwa sehemu alipozikwa baba yake hukohuko New Jersey.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








